15 February 2012

Madaktari wa Whitney Houston kuhojiwa

LOS ANGELES, Marekani

MADAKTARI wa Whitney Houston, watahojiwa kuona kama wanahatia kutokana na kutumia dawa mchanganyiko ambazo yanaelezewa kuwa pengine yalichangia katika kifo chake.

Nyota huyo inawezekana alikula kabla ya kukutwa akiwa bafuni katika hoteli mjini Los Angeles, ambako mwili wake ulikutwa, ilielezwa juzi.

Kwa Mujibu wa gazeti la The Sun, inahofiwa mwimbaji huyo alifariki kutokana na kutumia dawa nyngi za kutuliza maumivu na kuleta usingizi, pamoja na pombe kuliko kufa kwa kumeza au kuanguakia katika maji yaliyokuwa kwenye sinki la kuogea.

Nyota huyo wa filamu ya The Bodyguard alikutwa akiwa amekufa bafuni katika hoteli
ya Beverly Hilton Jumamosi ambapo uso wake ulikuwa ndani ya maji.

Bado haijajulikana kuhusu chanzo cha kifo chake.

Kwa mujibu wa taarifa, familia yake iliambiwa kuwa Whitney aliyekuwa na miaka 48, angeweza kufa kabla kutokana na kumeza dawa nyingi na kulewa pombe.

Juzi ilielezwa kuwa chupa za vidonge zilikutwa kwenye chumba chake zilikuwa
zimenunuliwa katika duka la dawa ambako zilikuwa zikinunuliwa dawa za marehemu Michael Jackson.

Askari wamesema kuwa dawa hizo zilitoka katika duka la dawa la Mickey. Ni sehemu ambako dawa alizokuwa akitumia Jacko aina
ya Demerol na nyingine zilitoka.

Kumekuwa na hisia kuwa pia mwimbaji Whitney alipatwa na matatizo ya moyo, ikiwa ni matokeo ya kutumia dawa nyingi.

Inaaminika kuwa kulionekana kiasi kidogo cha maji kwenye mapafu yake.

Polisi baada ya kupata kibali Los Angeles walifanya upekuzi kwenye chumba chake na kukuta vidonge vya aina sita Xanax, Lorazepam, Ibuprofen, Midol, Amoxicillin na Valium.

Wakati huohuo, picha zilizopatikana juzi zilionesha mlo wa mwisho aliokula Whitney muda mfupi kabla ya kifo chake ambavyo ni mchanganyiko wa mkate, nyama na mboga, viazi na pilipili huohuo ambapo alikula kidogo.

Wachunguzi wa vifo wa mochari ya County wataomba nakala ya rekodi ya utumiaji dawa  wa Whitney, limesema gazeti la The Sun.

Polisi inaweza kumfungulia mashtaka mtu yetote, atakayebainika kumpatia Whitney
dawa isivyo halali kabla ya kifo chake, jambo ambalo lilifanya baada ya kifo cha Michael Jackson aliyefariki Juni 25,2009.


No comments:

Post a Comment