Na Mwali Ibrahim
KATIBU Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Kashinde Shabani amesema watahakikisha timu ya taifa ya mchezo huo inafuzu kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Juni, mwaka huu nchini Uingereza.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu huyo alisema wanaimani watafuzu katika mashindano ya Afrika ambayo yatatoa wachezaji watakaokwenda Olimpiki.
Alisema mashindano ya kufuzu Olimpiki, yanatararjia kufanyika Aprili Mosi hadi 8 mwaka huu mjini Casablanka, Morroco.
"Ninainami hiyo, kwani wachezaji wetu wapo katika ari ya kutaka kufanya vyema kwenye mashindano yote ya kufuzu na hatimaye Olimpiki kwa kuwa wanajifua vya kutosha," alisema.
Alisema katika kambi ya timu hiyo kuna wachezaji zaidi ya 40, ambao wapo katika kambi mbili tofauti Zanzibar na Tanzania Bara.
Shaban alisema, wachezaji hao wanatarajia kukaa kambi ya pamoja Machi 8, mwaka huu lakini bado hawajajua kambi hiyo itakuwa sehemu gani.
Alisema wanataka kuiweka timu katika kambi ambayo itakuwa haina usumbufu kwa wachezaji hadi siku ya kuondoka.
No comments:
Post a Comment