10 February 2012

Kesi ya Mbunge Lema yaanza kuunguruma

Na  Queen Lema, Arusha

KESI ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema, imeanza kusikilizwa jana.

Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo upande wa mlalamikaji, Bw. Musa Mkangaa, aliieleza Mahakama jinsi Bw. Lema alivyotumia maneno kumdharirisha aliyekuwa mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.  Batilda Buriani.

Kesi hiyo namba 13 ya mwaka 2010, inasikilizwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na Jaji Mfawidhi, Gabriel Rwakibarila, kutoka Mahakama ya Sumbawanga.

Bw. Mkangaa alidai kuwa yeye binafsi alifanikiwa kutembelea sehemu nne za mikutano ya kampeni ya Bw. Lema, ambapo mbali na kutoa ahadi, mbunge huyo alimkashifu Dkt. Buriani.

Alidai kuwa Agosti 312010, katika eneo la Kwa Muorombo, Kata ya Terrat, Bw. Lema aliwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni kuwa wanaume katika makabila ya Wachaga na Waarusha, hawawezi kutawaliwa na mwanamke.

Alisema kauli hiyo kwa mujibu wa sheria ni kinyume cha taratibu na kudai kuwa, mbali ya kuwakataza wananchi kutompa kura Bi. Buriani pia aliwataka kujiadhari na watu wanaovaa vitambaa katika vichwa vyao, kwani huenda ni miongoni mwa makundi ya kigaidi.
 
“Mimi nilimsikia Bw. Lema akiwaambia wananchi wasimchague Dkt. Buriani kwa kuwa anavaa vitambaa na kufunika kichwa kila mara hivyo si kiongozi bora,” alisema.
 
Katika hatua nyingine, shahidi huyo alisema Septembe 18,2010, saa sita mchana katika eneo la Mbauda, Bw. Lema, akiwa na viongozi wa chama chake waliendelea kurudia maneno hayo.
 

2 comments:

  1. Lema ni kama mhuni wa stendi!

    ReplyDelete
    Replies
    1. mhuni angechaguliwa kuwa mbunge? ! wewe nawe umefulia

      Delete