Kuwania tenda ya ujenzi wa Daraja la kisasa la Kigamboni, Dar es Salaam baada ya kuthibitishwa kuwa na vigezo vilivyotakiwa.
Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Tenda ya ujenzi wa daraja hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha, katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii (NSSF) Bw. Ludovick Mrosso, makampuni hayo yameingia kwenye droo ya mwisho itakayotoa mshindi hivi karibuni.
Amesema bodi ya tenda ilikutana na makandarasi kutoka kwenuye kampuni hizo, pamoja na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana na kuonesha vielelezo vitakavyowaingiza kwenye mchakato wa mwisho.
Amesema awali Kampuni saba za ujenzi zilijitokeza na kuomba tenda ya kujenga daraja la Kigamboni, baada ya kutakiwa kuthibitisha uwezo wa fedha wa kampuni hizo, mbili zilijitoa na tano kuthibitisha kuwa na vigezo vilivyotakiwa.
Bw. Mrosso amezitaja kampuni hizo na kiwango cha fedha kuwa ni Long Jian Road and Bridge Ltd sh. 193,967,384,892.00, Schuan Road and Bridge Group Co. Ltd sh. 184,550,450,358.00 na China Communication Constructon Coy Ltd sh. 384,133,471,880.00.
Amezitaka kampuni nyingine kuwa ni China Railway Construction Engineer Group na China Major Bridge Engineer Co Ltd sh. 214,407,526,862/80 na Chong Qung sh.226,943,689,913.
Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi John Msemo, amefafanua kuwa baada ya kampuni hizo kuthibitisha kuwa na uwezo wa akiba ya fedha za kuanza ujenzi, Kamati itakutana na kupitisha jina la kampuni itakayoanza ujenzi wa daraja hilo.
Mhandisi Msemo amesema, watanzania hususan wakazi wa Kigamboni wana shauku ya kuona daraja hilo linajengwa kwa wakati, hivyo kamati itahakikisha Mkandarasi anayeshinda, anafanyakazi hiyo kwa wakati uliopangwa.
"Ni matarajio yetu kuwa wakandarasi watakayeshinda tenda ya ujenzi wa daraja la Kigamboni watafanyakazi hiyo kwa ufanisi na wakati uliopangwa, haraka iwezekanavyo", amesisitiza Mhandisi Msemo.
No comments:
Post a Comment