Na Mwali Ibrahim
BONDIA Francis Cheka, amesema ushindi alioupata katika pambano lake na Karama Nyilawila umezidi kumuonesha njia ya kushinda katika mapambano mengine yanayofuata.
Cheka na Nyilawila walizipiga mwishoni mwa wiki iliyopita katika pambano lisilo kuwa la ubingwa la uzito wa kg. 75 lililofanyika kwenye Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro ambapo Cheka alishinda kwa pointi 2.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Cheka alisema mwanga huo utampa mafanikio katika pambano lake la ubingwa wa IBF dhidi ya Mada Maugo, litakalofanyika Aprili 28 mwaka huu katika Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
"Nadhani kila mtu anaujua uwezo wa Nyilawila kwani amewahi kunyakua ubingwa wa Dunia wa WBF, lakini nilimpiga katika pambano letu hivyo naimani nitafanya hivyo hata kwa Maugo kwani njia tayari nimeoneshwa," alisema.
Alisema atakachokifanya katika pambano hilo ni kuongeza mazoezi kwani wakati akisubiri kupambana na Nyilawila, alijiandaa vya kutosha.
Aliongeza kuwa alifurahishwa kucheza na kuibuka mshinda kwa Nyilawila, ikinzingatiwa alikacha kutetea ubingwa wa WBF, ambao alikuwa akiushikilia.
No comments:
Post a Comment