03 February 2012

Timu 10 zathibitisha kucheza netiboli

Amina Athumani

TIMU 10 za netiboli, zimethibitisha kushiriki mashindano ya Ligi Daraja la Kwanza inayotarajia kuanza Februari 25, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Timu zilizothibitisha kushiriki michuano hiyo ni Rukwa, Mtwara, Lindi, Tandaimba, Manispaa Lindi, Prisons Mtwara, JKT Kigoma, Manispaa Sumbawanga, Rasi Lindi, Kurugenzi Wilaya ya Lindi na Polisi Sumbawanga.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Rose Mkisi alisema bado timu zaidi zinatakiwa kuthibitisha mashindano hayo.

Alisema kila mkoa unatakiwa kutoa timu mbili ili kushiriki mashindano hayo hivyo idadio ya timu zilizothibitisha ni ndogo ikilinganishwa na mikoa iliyopo.

Alisema timu zote zinatakiwa kuthibitisha hadi ifikapo Februari 20 mwaka huu ili kutoa nafasi kwa CHANETA kuandaa ratiba ya mashindano hayo .

Alisema mashindano hayo yatazipandisha daraja timu tatu za juu zitakazofanya vizuri na kuzipeleka ligi daraja la kwanza na kuzishusha timu tatu kutoka katika ligi daraja la kwanza.

CHANETA imewaomba wadau na makamupuni kujitokeza ili kudhamini mashindano hatyo ambayo kwa kiasi kukubwa yanachipua vipaji vipya vya mchezo huo.

mwisho

No comments:

Post a Comment