16 January 2012

Ward, Laura wasubili droo michuano Australia

Melbourne, Australia

WACHEZA tenis James Ward na Laura Robson, wamepenya hatua za awali ya michuano ya Wazi ya Australia na sasa wanasubili droo kubwa ya michuano hiyo.

Ward mwenye miaka 24 alimfunga Mholanzi Igor Sijsling kwa seti 7-6 (7-5) 6-2 na kufuzu hatua hiyo kwa mara ya kwanza akiwa nje ya nchi yake ya Uingereza.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), mchezaji huyo ameonekana mara mbili katika michuano ya Wimbledon, akipoteza mechi ya raundi ya kwanza 2009 na 2011.

Laura mwenye miaka 17, alimfunga Olga Savchuk wa Ukrain kwa seti 6-1 7-6 (7-2) ndani ya dakika 75 minutes.

Alionekana kuwa na ujuzi zaidi ya mara tatu wakati akicheza michuano ya Wimbledon na alifika hatua ya pili ya michuano ya Wazi ya US mwaka jana.

Mchezaji huyo alitumia wiki mbili Novemba za kuwa majeruhi baada ya dalili za awali kuonesha kuumia ubavu wake wa kushoto.

“Nimeingia katika mashindano nikiwa sina matarajio yoyote kutokana na kucheza nikiwa nahitaji pointi hasa katika siku tano za kwanza kabla ya mechi yangu ya ufunguzi,” alisema Laura na kuongeza;

“Ni mara yangu ya pili kufanya hivi ambapo kwangu ni vizuri na mechi mbili za mwisho nilizocheza, nilishinda katika raundi ya kwanza na katika droo itakayokuja nina imani nitafanya vizuri zaidi,” alisema.

Ward ambaye kwa ubora duniani yupo nafasi ya 161 alisema; "Ni siku ya furaha kwangu, nilikuwa na mechi ngumu sana, nilikuwa na seti tatu ngumu, hivyo najivunia kucheza vizuri leo,”.

"Kila wakati uanpotoka nje unaamini kwamba lazima utashinda lakini si kwa kila wiki,kutokana na kukutana na wachezaji wazuri zaidi, na mara nyingi huwa namuangalia Andy [Murray] nini anafanya na mafanikio anayoyapata katika kila mechi,”. Alisema.

Wachezaji wote watapangiwa wapinzani wao mara baada ya kukamilika kwa mechi hizo za awali.

Kuna wachezaji sita kutoka Uingereza waliokuja kushindana Melbourne, ambao ni Murray, Elena Baltacha, Heather Watson na Anne Keothavong ambao tayari wapo katika droo.

No comments:

Post a Comment