16 January 2012

BMT yatakiwa kuwawezesha mabondia

Na Andrew Ignas

BONDIA wa zamani wa timu ya Taifa ya Ngumi za Ridhaa Tanzania, Michael Yomba yomba amelitaka Balaza la Michezo la Taifa (BMT), kuhakikisha linatafuta njia mbadala ya kuwawezesha mabondia wao.

Akizungumza na Dar es Salaam hivi karibuni, Yombayomba alisema baraza hilo linatakiwa kutafuta njia mbalimbali kuwapa nguvu wachezaji wa timu hiyo ili wajitoe kwa nguvu moja kupigania maendeleo ya nchi.

"Viwango vya Mabondia wengi wa timu ya Taifa ya mchezo wa ngumi vinateremka kila kukicha, na hii inatokana na kutokuwa na ushirikiano kwa idara husika hususani kama BMT,"alisema Yombayomba.

Alisema kuwa mchezo wa ngumi umekuwa ikusahaulika licha ya kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kulipa sifa kubwa taifa ambapo medali mbalimbali zililetwa nchini kutokana na mchezo huo.

"Sifikili kama kuna mchezo uliolipa ambao umelijengea taifa jina kama ngumi, sijisifii lakini huo ndio ukweli ambapo mimi na Gogopoa na wengine ni baadhi ya mabondia ambao tulifanya vizuri sana,” alitamba bondia huyo.

No comments:

Post a Comment