* Wasema amevunja makubaliano waliofikia Ikulu
* Walituhumu Bunge kupenyeza vifungu 'kinyemela'
* Wajipanga kuhamasisha wananchi kuwaunga mkono
Na Benjamin Masese
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kusaini muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba Mpya 2011, Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na kupinga hatua hiyo kwa madai kuwa amekiuka makubaliano yao waliyofikia Ikulu Novemba 28, mwaka huu.
Pia chama hicho kimesema haitashiriki kwa namna yoyote wala kutoa ushirikiano katika mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na wadau wengine juuya Katiba Mpya kwa madai kuwa sheria iliyosainiwa na Rais Kikwete ni haramu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Makao Makuu ya CHADEMA Dar es Salaam jana,
Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. John Mnyika, alisema wamesikitishwa na hatua ya Rais Kikwete kukiuka makubaliano yao na kuamua kusaini muswada huo kabla ya kufanyiwa marekebisho.
Alisema kutokana na hali hiyo wametangaza rasmi kuanza mikutano ya hadhara na ya ndani kupinga maamuzi hayo hadi hapo marekebisho yatakapofanyika kama walivyokubalianoa Ikulu.
“Rais amesaini muswada wa sheria jana kabla ya kutekeleza makubaliano yetu, kuanzia sasa itakuwa sheria, sisi kama CHADEMA hatuko tayari kushiriki kwa kuwa sheria ni haramu.
Kamati kuu imewaagiza wabunge, viongozi na wananchi kuanza kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara mpaka kieleweke, pia bunge lijalo kitaeleweka,”alisema Bw.Mnyika.
Alidai kuwepo kwa uwezekano wa uvunjifu wa amani kutokea kwa kile alichodai kuwa ni bunge kuongeza kifungu cha 18 na 19 katika muswada huo na kupitishwa na bunge huku ikimkataza mwananchi au mtu yeyote kufanya shughuli au kuratibu au kutoa elimu juu ya mchakato wa Katiba Mpya wakati huu.
Alisema kifungu hicho kinatamka adhabu kati ya sh. milioni tano hadi 15 au kifungo jela kwa miaka mitatu hadi saba au vyote kwa pamoja na kwamba kifungu hicho kinakwenda kinyume na Katiba ya sasa ya nchi.
Alisema kifungu hicho kinakizana na ibara ya 18 katiba ya sasa inayompa mwananchi uhuru wa kutoa uhuru maoni sehemu yoyote juu ya jambo lolote na kudai kuwa wako tayari kwenda jela wote kwa ajili ya kutetea watanzania wote ili washirikishwe kupata katiba mpya waliyoipendekeza.
“Serikali imesaini muswada wa sheria, inakwenda kwa wananchi, na sisi CHADEMA tunakwenda kwa wananchi, tutakutana huko huko ndipo kitakapoeleweka na hata bungeni kitawaka, hatufanyi hivyo kwa maslahi ya chama chetu hapana, ni maslahi ya wote hata nyie waandishi mmenyimwa fursa pia ifahamike hatutafanya maandamano lakini mikutano lazima ifanyike,” alisisitiza.
Hata hivyo wamemtaka Rais Kikwete kutounda Tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba Mpya hadi hapo watakaporekesha kasoro zilizopo katika sheria na kutishia kuwa bila kufanya hivyo ni kukaribisha vurugu nchini.
Alisema kuanzia sasa watasambaza waraka uliokabidhiwa kwa Rais Kikwete na kile alichokiita kuwa ni maamuzi yaliyofikiwa nchi nzima ili wananchi wapate kusoma na kuona nani aliyekiuka makubaliano na kutoa maamuzi yao.
Bw. Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo Dar es Salaam alisema katika waraka waliomkabidhi Rais Kikwete ulimtaka kufanya mambo mawili ikiwa ni pamoja na kutumia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa ibara ya 97 ya katiba kutosaini muswada huo pamoja na iwapo mabadiliko ya msingi hayatafanyika hawako tayari kushiriki katika mchakato wa Katiba Mpya.
Kwa mujibu wa taarifa ya IKulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi jioni, kusainiwa kwa muswada huo ni hatua muhimu katika mchakato mzima wa Katiba Mpya.
Rais Kikwete aliweka wazi kuwa serikali ipo tayari kusikiliza na kupokea mawazo kwa lengo la kuboresha sheria hiyo. Pia katika mazungumza kati yake na Kamati ndogo ya CHADEMA Rais Kikwete aliwahakikishia kuwa serikali itaendelea kupokea maoni mbalimbali ya wadau ili kuboresha sheria hiyo kwa maslahi ya Taifa.
Rais Kikwete alisaini muswada huo kuwa sheria siku 11 baada ya kupitishwa na Bunge Novemba 18 mwaka huu mjini Dodoma huku wabunge wa CHADEMA wakiwa wameususia tangu mjadala wa muswada huo uliodumu kwa muda wa siku tatu na kutoka nje ya ukumbi wa bunge kwa maelezo kuwa hakubaliani nalo.
Baadaye CHADEMA waliomba kukutana na Rais Kikwete Ikulu kujadili suala ombi iliyojibiwa kwa kiongozi huyo kukubali na kukutana na ujumbe wa chama hicho ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bw. Freeman Mbowe, kwa muda wa siku mbili kisha pande hizo mbili kusaini makubaliano ya pamoja.
Pia hatua ya Rais kusaini muswada huo kuwa sheria baada ya kusikiliza maoni ya CHADEMA na kukubaliana nao huku akiweka wazi kuwa serikali ipo tayari kusikiliza maoni ya kuboresha zaidi sheria hiyo ilipongezwa na wasomi na wananchi mbalimbali kuwa ni hatua nzuri kwa maslai ya nchi.
Desemba 31, mwaka jana katika salamu zake za kufunga mwaka Rais Kikwete aliwaahidi watanzania Katiba Mpya kabla ya kumaliza muda wake wa utawala Kikatiba mwaka 2015 hivyo hatu iliyofikiwa sasa ni sehemu ya utekezaji wa ahadi hiyo.
Kusainiwa kwa muswada huo na kuwa sheria inatoa nafasi kwa Rais Kikwete kuunda Tume ya Kukusanya maoni ya wananchi kwa kushirikiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein.
Tayari Jeshi la Polisi lilikwishatangaza kutoruhusu maandamano au mikutano yoyote ya kisiasa kutokana na tishio la Kigaidi la kundi hatari la Al Shabab.
What do you expect from a man who can not run his own party? Pathetic! Hana msimamo,hana mwelekeo kigeugeu, and for that matter very incompetent. Thats your man JK
ReplyDeletei concur with you mr anony wa 12.08....
ReplyDeletekuwasikiliza chadema ilikuwa ni njia kuu ya kumsaidia jk...hata kutatua matatizoya ndani ya chama chake....
haya asiyesikia la mkuu!
Hakika hii itakuwa ni dhambi kubwa hasa kwa kiongozi anaye onekana kuwa kichwa ngumu, "any way" kitendo cha kuongeza vifungu ambavyo havikuwemo ili kuwatisha wananchi huu ni usaliti kabisa, hakuna mwenye kuweza kushindana na nguvu ya umma itakapo amua waongezee magareza maana raia wengi watafungwa.
ReplyDeletethe end is coming soon, that is the end of ccm
ReplyDeletekama nchi ni mali ya ccm na kikwete tutajua.mtatupiga risasi,mabomu na kutufunga kama kawa ama?
ReplyDeletetutaona nani mbuzi kati ya raiya na serikali.
punde si punde kama zambia na tuna hamu kinoma
CCM nyie ni Ma nincompo!.... mumechimba kaburi na mtajizika wenyewe. JK muda huo sijui atakimbilia wapi make hii sasa ni SODOMA NA GOMORA wananchi tuliisha hamasika sana na tutawaonyesha ubumbavu wenu wa kukubali maongezi na CHADEMA kisha munakiuka na KUFANYA UTHIRA.
ReplyDeleteMIMI NILISEMA MAPEMA HAO WACHAGA WANAKWENDA IKULU WATAKACHOZUNGUMZA HUMO NDANI SICHO WATAKACHOKUJAKISEMA NJE.NILIJUAA WATAGEUZA MANENO NA NDICHO KINACHOTOKEA. NILIMTAHADHARISHA MAPEMA RAIS WANGU KIKWETE AJICHUNGE SANA NA HAO MAFIA WANATAKA HAZINA YA NCHI KWA NAMNA YOYOTE ILE HATA KWA KUMWAGA DAMU. JE HAYAJATOKEA? WAMEPIGA MAPICHA NA RAIS NA KUPONGEZANA KUMBE WANA LAO JAMBO SASA WAMEGEUKA. HAWA MAFIA NI HATARI SANA. WATANZANIA TUJICHUNGE. KUNA FEDHA ZIMETOLEWA KUTOKA UMOJA WA ULAYA ZA KUELIMISHA JAMII KUHUSU MJADALA WA KATIBA MPYA SASA HAWA JAMAA NA WANAHARAKATI WAMEWEKA MKAKATI WA KUGAWANA.UFISADI HAUNA CHAMA JAMANI WOTE HAO WEZI TU
ReplyDeleteWEWE ANONYMAS WA 5.41, ACHA KUHUBIRI UKABILA. NYERERE AMETUJENGEA UMOJA WEWE UNALETA UKABILA HAPA. SHAME ON YOU.
ReplyDeleteHUNA HOJA, ONGEA HOJA KAMA MTANZANIA. INA MAANA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AMESAJILI VYAMA VYA UKABILA? KAMA NI HIVYO BASI MWAMBIE HUYO VASCO DA GAMA WAKO BASI AMFUKUZE MSAJILI WA VYAMA...
HIVI WEWE UNAONA MFUMUKO WA BEI, UNAONA WANAFUNZI HAWANA MIKOPO, SHILINGI HAINA THAMANI.
MBOWE ATAWEZA KUSIMAMIA MFUMUKO WA BEI? KAMA WACHAGA MNAVUSHA SUKARI KWENDA KENYA NA KUWAACHA NDUGU ZENU WA MOSHI WAKILANGULIWA SUKARI UNATEGEMEA NINI ? MFUMUKO WA BEI UTAPOTEA? NYIE NI MAFIA NA WEWE MWAMBIE HUYO COLUMBAS WAKO KAMWE NCHI HII HAITAMPA HAZINA MWIZI. TUNAKATAA WEZI KISHA TUWAWEKE WEZI.HILO SAHAU. HATURUKI MKOJO TUKAKANYAGA MAVI.WATANZANIA WENZANGU TAHADHARINI NA HAWA WACHAGA. SHILINGI MMEIPOTEZA SHILLINGI KUTOKANA NA WEWE KUPELEKA SUKARI KWA MAGENDO NJE NA KULIPWA PESA YA KIENYEJI BADALA YA DOLA. WEWE NDIO MUUAJI WA NCHI YAKO.
ReplyDeleteHIVI CHADEMA NDIO WANAAKILI KULIKO WATU WENGINE? HUU MSWADA KUSAINIWA NDIO UTATUPA SISIS FURSA YA KUJADILI NA KUWEKA YALE TUYATAKAYO NA KUYAKATAA TUSIYOYATAKA WAO WENDE WAPELEKE MAONI NA MAPENDEKEZO YAO KAMA CHADEMA KWA RIDHAA YA NANI KAMA SI WANA CDM PEKEYAO?WALIPOKATAA KUCHANGIA HOJA PALE BUNGENI WAMEKOSEA NDIO UKWELI TUNGESIKIA WANADAI NINI? WATUACHIE KATIBA NI MALI YETU TUTAIJADILI WAO WAKAE PEMBENI WAUNDE YAO SIJUI KWA RIDHAA YA NANI!!NA WAKISHAIANDIKA HIYO YAO ITATUMIKA WAPI?AU WAKIJA SHIKA DOLA?WASITAKE KUWAPOTOSHA WATU TUUNGANE KUWAELIMISHA WANANCHI NINI KINATAKIWA KUJADILIWA NA KUHAMASISHA WATU WENGI WAJITOKEZE,
ReplyDeleteWAACHE UNAFIKI WA NDUMILA KUWILI!!
TUMUACHIE RAIS WETU ACHUKUWE MAMLAKA YAKE NA TUSIMFANYE KAMA VILE NI KIONGOZI ASIEJUA WAJIBU WAKE.. CHADEMA WANAONEKANA HAWAJUI HATA UTARATIBU WA KUONGOZA NCHI, KWANI SI KILA ANETOKA VICHOCHORONI NA MAAMUZI YAKE AMPELEKEE RAIS WETU APOKEE.. HUU SI UONGOZI..VYOMBO VIPO KAMA BUNGENI NK.. TUNACHOWAOMBA CHADEMA WASIPELEKE MAPENDEKEZO KIHUNI.. WAFATE UTARATIBU NA KUVITHAMINI VYOMBO VILIVYOPEWA BARAKA NA WANANCHI KAMA HILO BUNGE WANALOLIKIMBIA KILA SIKU.... WAACHE KUDHANI KILA WANALOLITAKA WAO LITAKUWA!!! WANAASHIRIA UDIKTETA..WAMECHELEW!!!
ReplyDeleteWANAUZUNGUMZA UKABILA KUHUSU WACHAGGA , WAGOGO, WADIGO, WAHA, WANYAKYUSA, WANDENGEREKO, WAMASAI, WAHAYA, WAGOGO, WAMAKONDE, WAYAO, WASUKUMA, WABONDEI ........ WAMAFILISIKA KIAKILI. UKABILA ULIMALIZWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERERE. NAHISI BAADA YA MIAKA ISIYOZIDI 30 WANAOZUNGUMZIA UKABILA HAWATAKUWA NA LA KUZUNGUMZA TENA UKABILA UTAKUWA UMETOWEKA. UKABILA NI KUTU YA CHUKI. WATANZANIA SIO MAZEZETA WANA AKILI ZA KUTOSHA KUTAMBUA HUKUNA KABILA LENYE CHUKI NA LINGINE. NENDA NCHI KAMA KENYA,NIGERIA,AFRICA KUSINI, ISRAELI HATA AMERIKA- MWAMERIKA MWEUPE ANAMWONA MWEUSI NI KAMA MTU WA SECOND CLASS NA MWEUSI ANAMONA MWEUPE HIVYO HIVYO. MAKABILA YOTE TANZANIA HAYANA CHUKI BAINA YAO, WANAOANA, WANASHIRIKI VIFO NA SHEREHE PAMOJA WANAJIUNGA NA VYAMA BILA KUBAGUA- MBONA CCM IMEJAA WACHAGGA? AU UNATAKA WACHAGGA WOTE WAINGIE CCM ILI UKIITE CHA WACHAGGA? KINACHOFUATWA KWENYE CHAMA NI SERA NA SIO MTU AU KABILA. KAMA NI MKAKATI WA KUUA VYAMA VINGINE BASI HAWA NZI WACHACHE WAMEUMIA. HAKUNA CHAMA AMBACHO HAKINA KABILA. NENDA MAKANISANI, MISIKITINI, MASHULENI NA KWENYE VYUO VIKUU KAMA UTASHUHUDIA UOZO HUO WA UKABILA. NAHISI WACHANGIAJI HAPO JUU HAWAELEWI MAANA YA DHANA YA UKABILA. WARUDI SHULE WAKAFUNDWE. KAMA MNATAFUTA VYEO KISIASA,KIRAHISI AU KICHUKI TAMBUENI KUWA MMEOZA NA KUGANDA KIFIKRA. WATANZANIA WA SASA NI WEREVU, WAMENDA SHULE NA WAMEELIMIKA SIO KAMA WA MIAKA YA 47. WATANZANIA HAWANA CHUKI ZA KIKABILA WANAPENDANA NA WATU WOTE DUNIANI, NENDA ULAYA, MAREKANI N.K. UTAPATA SIFA ZA MMTANZANIA.
ReplyDeleteWACHANGIAJI WENZANGU, NAOMBA TUJIKITE KWENYE SUALA LA KWENDA IKULU KUTAFUTA SULUHU NA SIO MAMBO YA UKABILA. KWANI ILITANGAZWA KUWA WACHAGGA WANGEENDA IKULU? MBONA CUF ILIPOKWENDA IKULU MCANGIAJI HAKUSEMA NI WASUKUMA WALIOENDA IKULU KWA KUWA LIPUMBA NI MSUKUMA? JE, CUF HAINA WASUKUMA? ACHENI UJINGA . TUMIENI BUSARA SIO KULETA MAMBO YA FIKRA ZA KITOTO. FICHENI MAKUCHA YENU KWA AIBU. NADHANI UKIMUULIZA HUYO ANANYMOUS KAMA YEYE NI WA KABILA LIPI HATASEMA. ATAONA AIBU KWA KUWA WATANZANIA TUMEFIKIA HATUA AMBAYO HATA KUTAJA KABILA NI AIBU KUBWA! MWAMBIE ANONYMOUS AFANYE MKUTANO NA AANZE KULISEMA KABILA FULANI NA HAPO NDIPO ATAKIONA NA MTEMA KUNI. YEYE ABAKIE NA CHUKI ZAKE.
ReplyDeleteWATANZANIA TUZIDI KUPIGANIA HAKI, TUSITETEE WEZI WALAFI WA KUJILIMBIKIZIA MALI HATA KAMA NI WA KABILA GANI. BILA KUFANYA HIVYO, HATUTASONGA MBELE.
LABDA ANONYMOUS ANATAKA WAZUNGU AU WAASIA WAJE KUONGOZA VYAMA VYA SIASA NCHINI NDIPO ATAONA HAKUNA UKABILA.
Du!mmetoka kabisa kwenye mada ndugu zangu,me naona tunahitaji mabadiliko ya kweli na utaifa tuuweke mbele.
ReplyDeleteTunahitaji kuelezwa udahaifu wa sheria iliyosainiwa ili tuweze kuamua hatua za kuchukua. Chadema na waandishi mliokuwepo tuelezeni ni kitu gani kimekosewa na jinsi gani tutatue kosa hilo. Naona CCM, CHADEMA na Vyama vingine na wananchi lengo letu ni moja...Katiba mpya. Tuonyesheni kasoro zilizoko ktk mchakato na jinsi zitakavyoathiri hiyo Katiba inayotarajiwa.
ReplyDelete