02 December 2011

Uchaguzi DAAA 'waota mbawa' tena

Na Amina Athumani

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), uliopangwa kufanyika kesho umepigwa tena kalenda kwa muda
usiojulikana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Michezo wa Mkoa wa Dar es Salaam Adoph Alii, alisema uchaguzi huo umesogezwa mbele kwa muda usiojulikana kutokana na sherehe za mwenge wa Uhuru.

Alisema pia kutokana na Wizara, Idara za Serikali na taasisi mbalimbali kukabiliwa na sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambazo nazo, imechagia kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

Alii alisema kutokana na hali hiyo wajumbe na wagombea wa uchaguzi huo, wanatakiwa kuvuta subira hadi uchaguzi huo utakapotangazwa upya.

Awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika Oktoba 23, mwaka huu lakini ulivunjika muda mchache baada ya wasimamizi, kugundua kuwa wapiga kura hawakuwa wajumbe halali.

No comments:

Post a Comment