02 December 2011

Bahati nasibu mpya yazinduliwa

Na Mohamed Kazingumbe

BODI ya Bahati Nasibu Tanzania, jana imezindua bahati nasibu ya taifa ya Winlot, ambayo itaanza kuchezwa katika mikoa ya
Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.

Akizinduza bahati nasibu hiyo, Mkurugenzi wa bodi hiyo, Abbas Tarimba alisema kampuni hiyo kuwekeza nchini ni faraja kubwa kuwa Watanzania watafaidika kwa kupta ajira kuptia Winlot.

Alisema kampuni hiyo, ambayo imefika katika nchi mbalimbali duniani licha ya kutoa ajira, pia itakuwa ikichangia huduma mbalimbali za kijamii.

"Licha ya Watanzania kufaidika na kampuni hii, pia itakuwa ikitoa asilimia 10 kwa ajili ya kusaidia michezo mbalimbali kupitia BMT (Baraza la Michezo la Taifa).

"Sasa fedha hizo itakuwa ni jukumu la BMT kusaidia michezo inayotaka japokuwa mimi ni mpenzi mkubwa wa mchezo wa mpira wa miguu, lakini hilo litakuwa jukumu lao wao," alisema Tarimba.

Tarimba aliwataka Watanzania kuchangamkia bahati nasibu hiyo ambayo itawafaidisha wengi likiwemo taifa, kwani kutapatikana ajira za kudumu zaidi ya 300 na kwa wadau binafsi zaidi ya 25,000.

Naye Mkurugenzi Masoko wa kampuni hiyo, Amani Honestus alisema kuwa njia mbalimbali zitatumika kuchezesha bahati nasibu hizo.

Alisema tiketi za bahati nasibu hizo zitauzwa kwa sh. 500 na droo yake itakuwa ikichezeshwa mara moja kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi.

ends.....





Tarimba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, aliongeza huduma hiyo inayorudi baada ya serikali kusitisha Bahati nasibu ya Taifa mwaka 2003, itakuwa moja ya kumbukumbu wakati taifa linaadhimisha kutimiza miaka 50 ya uhuru ifikapo Disemba 9.

Nguvu ya dhana ya Winlot kuchangia mfuko wa michezo ilidhirishwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la Makampuni ya Sugal& Damani, Kamlesh Vijay, ambayo ni kampuni mama ya Winlot ya India, aliimbia Majira kuwa kila waendepo, lengo lao ni katika kuinua huduma za jamii, michezo ikipewa kipaumbele.

Alisema Tanzania inayochukuwa nafasi ya pili barani Afrika kwa undeshaji mzuri wa michezo ya kubahatisha anaamini watafaidika sana katika ajira na huduma za jamii iwapo wengi watashiriki katika michezo yake.

"Tupo katika nchi nyingi duniani, mbali ya India, pia tupo, Uingereza, Kenya, Zambia, Nigeria, ambako kote tumepata mafanikio mengi sio tu kwa faida ya kampuni bali pia faida katika kuinua uchumi wa nchi husika kwa kodi na ajira kwa raia," alisema Vijay.

Akifafanunua aina ya michezo itakayochezwa Mkurugenzi wa Masoko wa Winlot Tanzania, Amani Honestus, alitaja njia mbalimbali za kuchezesha, ikiwa pamoja na tiketi tatu kuingia katika droo ya kila siku na kila wiki, kundi lingine ni aina ya Twiga 6/49 wa kila Jumamosi na kutoa zawadi hadi zaidi milioni kumi. Mchezo aina ya Duma/5/39, kuchezwa mara moja kila siku na zawadi hadi milioni kumi, na mwingine aina ya Simba 5/90 utkaochezwa mara tisa kila siku.

No comments:

Post a Comment