Na, Rashid Mkwinda, Mbeya
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameelezea masikitiko yake ya tishio la kuvunjika kwa umoja
na mshikamano wa Watanzania ambao ulikuwepo baada ya
kupata Uhuru na kusema kuwa
uwepo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ulisaidia kuwakutanisha watu wa itikadi
tofauti bila kujali rangi au jinsia.
Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 56 ya Jumuiya ya Wazazi nchini
sanjari na miaka 50 ya Uhuru,yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya
Wazazi Meta Bw. Pinda alisema msingi wa mshikamano ulidumishwa ndani ya Jeshi la
Kujenga Taifa JKT kwa kuwa hakukuwa na ubaguzi wa elimu wala cheo isipokuwa utaifa
ulitangulizwa mbele katika kudumisha umoja miongoni mwa Watanzania.
''Katika jambo tunalopaswa kujivunia katika miaka 50 ya Uhuru ni hili la Mwalimu
kutuunganisha kuwa kitu kimoja, katika Taifa moja lenye lugha moja na kila mtu ana
uwezo wa kwenda kokote bila kuulizwa ni kabila gani,''alisema Bw. Pinda.
Alisema kuwa wapo wanaodharau amani na utulivu uliopo wakidhani kuwa umekuja bila
mikakati makini ya waasisi wa Taifa hili na kuongeza kuwa wanaobeza amani na utulivu
wa nchi yetu hawawatakii mema Watanzania ambao wanajivunia miaka 50 ya Uhuru ndani
ya Umoja na Mshikamano.
''Msiwasikilize wanaodhani vurugu ndio suluhisho la matatizo ya nchi yetu..Vijana
msikubali kutumika katika maandamano yasiyo na tija, maandamano ya aina hii hayana
nia nzuri katika kudumisha amani ndani ya nchi yetu''alisisitiza.
Bw. Pinda alisema kuwa iwapo kuna jambo ambalo linapaswa kuwekwa sawa miongoni mwa
Watanzania ipo nafasi ya kukaa kujadili na kutafutiwa ufumbuzi badala ya kundi moja
la watu kuamua kuingia barabarani kwa kisingizio cha maandamano ya kudai haki.
Awali akizungumza katika hadhara hiyo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Bw.
Athumani Mhina alisema matukio ya maandamano yanayoitishwa na baadhi ya vyama vya
siasa yanapaswa kubezwa kwa kuwa yana kila dalili ya kusababisha uvunjifu wa amani.
Bw. Mhina alisema kuwa baadhi ya vyama hivyo vinatumia nguvu kubwa katika kufanya
maandamano badala ya kushiriki katika maendeleo na hivyo kuchangia kwa namna moja
ama nyingine kuchangia kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Wewe Pinda umedharaulika baada ya kuweka saini ya kuchukua sh 280,000/= ambazo zilichangishwa pasipo halali. Hata Libya walidhani kuna amani na utulivu mpaka watu walipoamka na kudai haki. Pasipo haki hakuna amani usidanganyike wala kudanganya watu!!!
ReplyDeleteWalibya wamelalanika na laana zao zitawaletea majibu sio muda mrefu na watavuna walichokipanda itakuwa maajabu ya dunia kupanda mahindi ukaja kuvuna mtama ukipanda shari utavuna shari sio heri walibya wanachokipigania sio maisha mazuri wanakila kitu kinacho liliwa na watanzania na nchi nyingine duniani wanachokipigania wao ni ukabila na udini na kama hiyo ndio sababu ya kuandaa maandamo yasio kwisha nchini na sisi wapenda amani tanzania tupo tayari kupigana mpana tonye la mwisho la damu kuhakikisha amani inadumu hata kama chama kinachotawala kitakuwa kinaibiya nchi tunachotaka kidumishe amani kwanza kabla hatujaushghulikaia ubadhirifu. Hongera Pinda mwana wa mkulima tuponyuma yako!
ReplyDeleteWeee! Nyuma ya Pinda unatafuta nini? Kaa mbele yake!
ReplyDeletewewe uliyoko nyuma ya pinda inaonekana wewe unatoka kwenye familia bora, uko kwenu kuna gari za zima moto za kubebea wagonjwa walinzi wa kila aina, umeme sio tatizo kwenu, barara ni nzuri, majumba mazuri, mnasoma amerika na ulaya asia, na baba zenu wana akaunti zilizo jaa pesa za walipa kodi huhuko mnakosoma, hivi kuna amani gani kwa watanzania? mzee nyerere alivitunza vitu vyote vyenye thamani kwa ajili ya watanzania kama dhahabu, ardhi, nk, lakini leo hivyo vitu vinauzwa kwa wageni wakishirikiana na hao kina pinda, watu wakilalamika mnaseama wanataka kuleta vurugu, mmeshachelewa hatutarudi nyuma mpaka kieleweke, na muingu yupo nasi
ReplyDeletemzee wangu pinda! naomba unijibu, kwa nini ukuwapeleka atoto wako kisoma shule za kata? kama wewe ni mzalendo wa ukweli, tunajua watoto wako wanaposoma ni shule ya hali ya juu sana, kwa hiyo tusitegemee kuwapata viongizi kutoka kwa watu masikini, tusipo jitaidi na kupambana tutatawaliwa na hao hao, hii tanzania ni nchi ya watu wote,
ReplyDeleteWatu wanaozungumzia amani katika hali ya maisha tuliyo nayo Tanzania kwa sasa wanaota. Mwanzoni sisi wakristu tulidanganywa eti ukilambwa kofi shavu moja toa shavu la pili. Yesu mwenyewe alipopigwa kofi na wabaya wake alin'gaka akisema kama hakujibu vibaya mbona alipigwa. Wenzetu wanaishi kwa jambia na jino kwa jino. Sasa hapa tunataka kieleweke. Tumechoka kuibiwa, kunyanyaswa, kutukanwa kunyimwa haki. Suluhu ni barabarani mpaka tone la mwisho. Wanaofaidi makombo ya wezi wajikalie nyumbani sisi sasa basi. Pinda, just shut up ugly face!
ReplyDeleteMshikamano utakuwapo vipi wakati nchi imegeuka ya walio nacho na wasionacho? Nchi itakuwa na mshikamano vipi wakati nchi imekuwa ya ufisadi mtupu na waliomadarakani hawataki kujirekebisha?
ReplyDelete