Na Mwali Ibrahim
MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Chaurembo Palasa na Venance Mponji wanatarajia kupanda ulingoni Desemba 24,
mwaka huu kuwania ubingwa wa Afrika utakaosimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Pambano hilo linatarajia kuwa la uzito wa kg. 61 la raundi 12, ambalo litafanyika katika Ukumbi wa DDC Keko, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Kaike Siraju, alisema maandalizi yanaendelea ambapo na mabondi wote wapo kambini kwa ajili ya kujiandaa kuwania ubingwa huo.
"Pambano hilo litachezwa usiku, ikiwa ni pamoja na kusheherekea mkesha wa sikukuu ya Krismas," alisema.
Alisema pambano hilo litatanguliwa na mapambano mengine kati ya Said Zungu na Seba Temba, uzito wa kg. 63, Simba Watunduru atachuana na George Sayuni kg. 57, Said Maulid na Kasim Tyson kg. 60 yote yatakuwa ya raundi sita.
Alisema pambano la Juma Fundi na Baina Mazola, litakuwa la raundi nane uzito wa kg. 52.
Kaike alisema pia kutakuwa na burudani ya mtindo wa kiduku itakayotolewa na wasani B Alone wa Njombe na GS wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment