27 December 2011

Matumla, Oswald hakuna mbabe

Na Mwali Ibrahim

MABONDIA Rashid Matumla na Maneno Osward, wametunishiana misuli na kutoka droo katika pambano lao lisilo la ubingwa lilofanyika katika Ukumbi wa
Heinken, Mtonikijichi, Dar es Salaam.

Pambano hilo lilikuwa katika uzito wa kati la raundi 10 ambapo mabondia wote waliweza kumaliza raundi zote huku wakitoshana nguvu.

Katika kutoshana nguvu huko, kuliwalazimu majaji kutoa pointi 99-99, hivyo kuwa hakuna aliyekuwa bingwa kati yao  ambapo kila bondia baada ya hapo alijitapa kumdunda mwenziwe.

Katika raundi zote, Matumla alionekana kuanguka kwa kila raundi kutokana na kudaiwa kutereza kwa ulingo huo kitu kilichomkera na kuwalaumu waandaaji kwa kutokuwa makini katika kuandaa ulingo.

'Ulingo ulikuwa mbovu kwani nilijikuta nikiangua kila mara hivyo kutaka kunipunguzia kasi ya kupambana lakini namshukuru mungu kwa kuweza kumaliza raundi zote ingawa tulitoka droo," alisema Matumla.

Naye kwa upaande wake, Oswald alisema ubingwa huo ulistaili kuwa kwake lakini anashindwa kujua nini kilichotokea hadi matokeo kuwa droo ingawa alijitaidi kuonesha uwezo mkubwa.

"Sababu za kutokupewa ubingwa huo sijui ni nini lakini nilistahili kuwa bingwa hivyo nawataka majaji wanapokuwa wanapanga matokeo yao wawe makini katika kuangalia nini bondia anakifanya," alisema Maneno.

No comments:

Post a Comment