Yainyuka Ethiopia 2-0
Na Speciroza Joseph
MICHUANO ya Tusker Challenge Cup, iliendelea tena jana ambapo Kenya, ilikurupuka usingizini na kuichapa Ethiopia mabao 2-0, katika mechi ya Kundi C iliyochezwa saa 8 mchana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kenya iliandika bao la kwanza dakika ya 11 kupitia Bob Mugalia, ambaye aliunasa mpira uliowashinda mabeki wa Ethiopia, kutokana na utelezi uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha jana mchana jijini Dar es Salaam.
Dakika ya 43 Pascal Ochieng wa Kenya aliipatia timu yake bao la pili, baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Ethiopia, kutokana na mpira wa kona uliochongwa na Kelvin Kimani.
Awali kabla ya bao hilo, Kenya ambayo jana ilionekana kuwa na uchu wa mabao Jamal Mohamed, alikosa penalti iliyotolewa na mwamuzi, Garvis Munyanziza wa Rwanda baada ya mabeki wa Ethiopia kumwangusha, Victor Ochieng katika eneo la hatari wakati akienda kufunga.
Kipindi cha pili kilianza kwa Kenya, kuendelea kuutawala mpira kwa kiasi kikubwa na kufanya mashambulizi mara kwa mara langoni mwa wapinzani wao, lakini washambuliaji wake hawakuwa makini katika kufunga.
Katika kipindi hicho Ethiopia walionekana hawako sawa, lakini walitengeneza nafasi chache ambazo hata hivyo, hawakuweza kuzitumia vyema.
Timu zote zilifanya mabadiliko, ambapo Ethiopia iliwatoa Alula Girma, Ayenalem Hailu na Shemeles Godo na kuwaingiza Tesfaye Bekele, Mikael Kena na Dawit Fekadu.
Kenya nayo iliwatoa Kelvin Kimani na Victor Ochieng na wakaingia, Steven Waruru na James Atudo.
Mabadiliko hayo kidogo yaliisaidia Ethiopia, ambapo wachezaji wake Adane Gabreyes na Gatene Kabede walikosa mabao ya wazi wakiwa katika nafasi nzuri za kufunga dakika za 69 na 74.
Kwa matokeo hayo Kenya ambayo ilifungwa mabao 2-0 na Malawi, ambayo ni timu mwalikwa katika mechi yake ya kwanza imetoka na pointi tatu, huku Ethipoia wakibakiwa na pointi moja.
Katika mechi ya pili iliyochezwa saa 10 jioni katika uwanja huo, Sudan na Malawi zilishindwa kutambaina, baada ya kutoka suluhu
No comments:
Post a Comment