01 December 2011

Ruvu yatafuta mechi za kirafiki

Na Shufaa Lyimo

TIMU ya Ruvu Shooting imepanga kucheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, utakaoanza kutimua vumbi Januari mwakani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Dar es Salaam jana, Msemaji wa timu hiyo, Masau Bwire alisema katika usajili wao wameongeza wachezaji watatu, ambao wataziba mapengo yaliyopo.

Alisema wachezaji waliosajiliwa ni nafasi ya kipa na washambuliaji wawili.

"Hivi sasa tunatafuta mechi za kirafiki, ambazo zitatusaidia kuona upungufu ambao benchi la ufundi litaufanyia kazi," alisema Bwire.

Alisema timu hiyo iliingia kambini tangu Novemba 12, mwaka huu wakiamini kuwa mzunguko ujao utakuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa kila timu, imepata nafasi ya kujiandaa vyema.

"Tulianza kambi tangu Novemba 12, tumeamua kufanya maandalizi mapema kwa sababu tunafahamu ugumu utakaokuwepo kwenye ligi hiyo," alisema.

Naye Kocha Msaidizi wa timu hiyo Selemani Mtungwe, ambaye kwa sasa ana jukumu la kuinoa timu hiyo baada ya Kocha Mkuu Boniface MKwasa, kuwa na Kilimanjaro Stars inayoshiriki michuano ya Chalenji Dar es Salaam alisema kikosi chake kiko tayari kwa ligi hiyo.

Katika msimamo wa ligi Ruvu Shooting ipo katika nafasi ya nane baada ya kujikusanyia pointi  15.

No comments:

Post a Comment