Na Lilian Justice,
Morogoro
KAMPUNI ya Zana za Kilimo Tawi la Morogoro imeamua
kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete la ’Kilimo Kwanza‘ katika kutekeleza agizo hilo kwa vitendo zaidi.
Hayo yalielezwa jana na Meneja wa kampuni ya kampuni hiyo Bw. John Mwapili wakati akizungumza na Majira.
Bw. Mwapili alisema kuwa Kampuni ya hiyo imeamua kutekeleza azama ya kusukuma sekta ya kilimo mkoani hapa ili kuwawezesha wakulima kutekeleza agizo la serikali kuteua mkoa wa Morogoro kuwa Ghala la Chakula la Taifa.
Pia Bw. Mwapili alisema kuwa kampuni imeshaleta zana mbalimbali za kilimo katika
tawi hilo yakiwemo matrekta ya aina mbalimbali ya kulimia na kuvunia na pi palizi.
Aidha alibainisha kuwa matrekta hayo ni pamoja na matrekta madogo maarufu kama
‘Power Tillers’
Hata hivyo uteuzi wa Mkoa wa Morogoro kuwa Ghala la Chakula la Taifa ulitokana na hali ya mvua za uhakika za msimu wa kilimo maeneo makubwa ya ardhi yenye rutuba isiyohitaji mbolea.
No comments:
Post a Comment