LONDON, Uingereza
KLABU ya Fulham, imetolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Europa sambamba na timu ya PSG ya Ufaransa. Timu hiyo ya Ligi Kuu England, ilianza mechi huku ikiwa ni
kinara katika kundi lake kwa kuwa mbele kwa pointi moja, dhidi ya timu ya Poland Wisla Krakow, ikiwa na maana kuwa ushindi ungetosha kuwavusha katika hatua ya mtoano ya mashindano hayo.
Walikuwa na uhakika wa kuondoka na pointi zote tatu, hadi kufikia mapumziko baada ya kupata magoli kupitia kwa Clint Dempsey na Kerim Frei.
Lakini Odense, iliyokuwa haina nafasi ya kusonga mbele iliendelea kupambana na dakika ya 64 mpira wa adhabu wa Hans Andreasen, ulimpita kipa wa Fulham, Neil Etheridge.
Fulham ingawa ilikuwa ikihitaji ushindi tu, ili kujihakikishia kusonga mbele lakini ilicheza mpira wa kujihami na katika dakika za mwisho, mambo yaliharibika.
Kwa mujibu wa The Sun, mshambuliaji kutoka Senegal, Baye Djiby Fall alipiga krosi ya nguvu na kuifanya Odense kusawazisha na kuwatuliza wenyeji.
Kutokana na Wisla Krakow, kuifunga FC Twente mabao 2-1 ambayo ilishajihakikishia kusonga mbele, timu ya Polandi ndiyo iliyopenya katika Kundi K.
Katika Kundi F, PSG ilitolewa katika mashindano hayo licha ya kuifunga Athletic Bilbao, mabao 4-2.
No comments:
Post a Comment