BUENOS AIRES,Brazil
KOCHA wa zamani wa timu ya Taifa ya Argentina, Carlos Bianchi,amesema kwamba hana wasiwasi na kiwango alichonacho nyota wa Barcelona, Lionel Messi,na amesema kwamba kwa sasa mchezaji huyo ameshawapiku wachezaji nyota wa zamani Diego Maradona na Pele.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa AFP,mkufunzi huyo wa zamani ambaye klwa sasa yupo nje ya soka baada ya kuacha kuzifundisha timu za Boca Juniors na Velez Sarsfield,alitoa kauli hiyo juzi zikiwa ni siku chache baada ya nyota huyo kuisaidia Barcelona kutwaa ubingwa wa dunia baada ya kuilaza Santos kwenye mechi ya fainali.
"Siku chache zilizopita nilizungumza kitu kama hiki, baada ya Wabrazil kuniuliza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu ni mchezaji gani bora katika historia ya soka kati ya Maradona ama Pele.Nilichowajibu NI kwamba kwa kuwaheshimu wote wawili nilisema kwamba kwa sasa ninayemuona ni bora ni Messi,"alisema kocha huyo.
Bianchi vilevile hakusita kuimwagia sifa timu nzima ya Barcelona, ambapo alisema kwamba ndiyo inayoonekana kuwa ni tishio uwanjani..
"Soka lililooneshwa na Barcelona ilipoichapa Santos,lilinifanya niweze kutoa kauli kama hiyo,kwa sasa timu hiyo ipo kwenye kiwango cha hali ya juu," alisema.
No comments:
Post a Comment