22 December 2011

Madrid yatinga 16 kwa kishindo

MADRID,Hispania

TIMU ya Real Madrid imesonga mbvle kirahisi kwenye michuano ya Kombe la Mfalme maarufu kama Copa del Rey  baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1  dhidi ya timu inayocheza ligi daraja la tatu Ponferradina, huku timu za  Sevilla, Espanyol na Mallorca nazo zikisonga mbele baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao.
Alikuwa ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Hispania, Jose Callejon aliyewafanya mabingwa hao  kupata ushindi wa tatu mfululizo na pia kuifanya timu hiyo ya Santiago Bernabeu kusonga mbele  katika hatua ya 16 kwa jumla ya mabao 7-1.

Callejon alipachika bao lake la kwanza dakika ya 25 baada ya kumchambua mlinda mlango  Orlando Quintano.


Mchezaji Nuri Sahin, ambaye alipata fursa ya kuanza baada ya kocha, Jose Mourinho kuwapumzisha wachezaji Cristiano Ronaldo, Xabi Alonso na Angel di Maria, alipachika bao lake dakika ya 44 baada ya kujitwisha mpira wa kona iliyochongwa na  Oezil,

Quintano alipachika baoa la tatau dakika ya 49 baada ya kuunganisha mpira wa adhabu iliyochongwa na mchezaji  Raphael Varane,kabla ya Acoran Barrera kuwafungia wagenmi baoa la kufutia machozi dakika nne baadaye.

Alikuwa Joselu Mato aliyeipatia Real Madrid baoa la nne dakika ya 79,baada ya kutokea benchi kati ya wachezaji wanne kutoka timi B waliotumiwa na  Mourinho kabla ya Callejon kupigilia msumlai wa mwisho kwa mpira wa adhabu.

No comments:

Post a Comment