22 December 2011

Korea Kusini yapata kocha mpya

SEOUL,Korea Kusinbi

KOCHA wa mabingwa wa ligi,Jeonbuk Hyundai Motors,Choi Kang-Hee,ametangazwa kuwa ndiye kocha mpya wa timu ya Taifa ya Korea Kusini.
Shirika la Habari la Ufaransa AFP,lilinukuu Shirikisho la soka la nchi hiyo likieleza  kwamba Choi atakuwa akichukua nafasi ya aliyekuwa kocha  mkuu wa timu hiyo, Cho Kwang-Rae, ambaye alitimuliwa wiki mbili zilizopita baada ya timu hiyo kuambulia kipigo kisichotarajiwa kutoka kwa Lebanon ambacho kimewaacha wananusufainali wa mwaka 2002 kuingia hataribni kuzikosa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014.

Choi, 52, mara mbili amewahi kuiwezesha, Jeonbuk kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo mwaka  2009 na  2011, huku akiiwezesha timu hiyo pia kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Asia mwaka 2006  na huku mwaka huu ikimaliza michuano hiyo ikiwa mshindi wa pili.

Kwa sasa Korea Kusini inasaka kuonekana kwa mara ya nanae mfululizo katika michuanoi ya Kombe la Dunia.

Vinara hao wa kundi B kwa upande wa Asia kwa sasa wana pointi 10 sawa na Lebanon na wapo mbele dhidiu ya Kuwait ambayo inashika nafasi ya tatau ikiwa na pointi nane.

No comments:

Post a Comment