18 November 2011

Yanga yapata ushindi wa kwanza

Na Shaban Mbegu

BAADA ya kuanza vibaya katika mashindano ya vijana ya Uhai Cup, timu vijana ya Yanga jana ilizinduka na kupata ushindi wa kwanza wa mabao 2-0 dhidi ya Polisi Dodoma.


Yanga katika mashindano hayo ilinza kwa kufungwa na Moro United, kabla ya kupoteza tena mchezo wa pili dhidi ya Villa Squad.

Katika mchezo huo, ambao ulifanyika katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam Yanga ilionekana mapema kutaka kurekebisha makosa yake.

George Banda ambaye alikuwa katika kiwango kizuri alitumia uzembe wa mabeki wa Polisi na kuipatia Yanga bao la kwanza.

Bao hilo lilionekana kuwashtua Polisi, ambao walianza kucheza kwa kasi lakini walikutana na upinzani mkali kutoka kwa walinzi wa Yanga.

Said Mohamed ambaye ni beki wa kati ya Yanga aliipatia timu yake bao la pili dakika ya 17 na kufuta matuamini ya Polisi, kusawazisha katika kipindi cha kwanza.

Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko Yanga ilikuwa inaongoza.

Kipindi cha pili kilinza kwa kasi huku kila timu ikionekana kutaka kupata mabao, lakini mapaka dakika 90 zinamalizika Yanga walitoka na pointi tatu.

Katika mchezo wa juzi jioni, Simba ilionja kipigo cha kwanza kutoka kwa Toto Africa ya Mwanza, ambapo bao la Toto lilifungwa na Phaby Ngwase.

No comments:

Post a Comment