18 November 2011

Tumepiga hatua kubwa sekta ya afya- Wizara

Na Riziki lupatu

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imejitamba kuwa licha ya kuwepo kwa onhezeko kubwa la watu imepata mafanikio makubwa katika uboreshaji wa sekta ya afya nchini katika kipindicha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari wa wizara hiyo Dar es Salama jana, kumekuwepo kwa upanuzi na maboresho katika huduma za afya kwa kipindi cha miaka 50 ya uhuru ikilinganishwa na miaka 70 ya ukoloni.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa vifo vya watoto wachanga vimepungua kwa kiasi kikubwa kutoka wastani watoto 522 kati ya 3,000 hadi kufikia vifo 158 kati ya 3,000 kwa sasa hatua amabyo ni kubwa kwa nchi masikini kama Tanzania.

Taarifa hiyo pia inasema ongezeko la vituo vya kutolea huduma za afya  vimeongezeka kutoka 1,343 mwaka 1961 hadi kufikia 7,336 katika kipindi cha mwaka 2010/2011.

Wizara hiyo pia imesema wastani wa madaktari wanaohitimu kwa mwaka imeongezeka kutoka madaktari 50 mwaka 1961 hadi Madaktari 600 katika kipindi cha mwaka 2010/2011.

Hata hivyo imeelezwa kuwa bado kuna changamoto nyingi zinazokwenda sambamba na mafanikio hayo ya sekta ya afya.

Baadhi ya changamoto hizo ni uwendeshaji wa huduma za Afya na Ustawi wa jamii kwa ujumla, uelimishaji na upashanaji habari na uzingatiaji sera, Miongozo, Sheria, kanuni, Mipango na Mikakati.

Baadhi ya vipaumbelem katika kuboresha huduma za Afya na nchini ni pamoja na kuimarisha udhibiti wa magonjwa yanayoambukizwa, yasiyoambukizwa pamoja na yale yaliyosahaulika. Pia kuvijengea uwezo vituo vinavyotoa huduma za Afya na Ustawi wa Jamii.

Hata hivyo huduma za afya hususan katika vituo vya serikali bado imeendelea kuwa kero kubwa kwa wananchi kutokana kile kinachodaiwa kuwa ni upungufu wa watumishi, vifaa tiba, vitendea kazi vingine kama magari, majengo, vitanda na mashuka.

No comments:

Post a Comment