11 November 2011

Waziri Mkuu Pinda -Atoa Ufafanuzi kuhuse Mheshimiwa Lema

Wakati huo huo Waziri Mkuu Pinda amekiri kwamba serikali ipo katika harakati mbalimbali za kuhakikisha kwamba inatafuta ufumbuzi wa

migogoro inayoendelea mkoani arusha ambayo hivi karibuni ilisababisha mbunge wa jimbo hilo Bw. Godbless Lema, na wenzake kukamatwa na kufikishwa  mahakamani.

Bw. Pinda alisema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Steven Ngonyani (CCM) maarufu kama Profesa maji marefu aliyetaka kujua  kauli ya serikali juu ya hatima ya mgogoro huo pamoja na sababu za kunyimwa dhamana kwa Bw. Lema kutoka gerezani.

"Mheshimiwa Spika ni kweli kwamba pale Arusha kuna migogoro mingi imekuwa ikijitokeza mara kwa mara, sisi Watanzania tunapaswa kujiondoa huko kabisa kwa sababu siyo jambo la kujisifia, ndiyo maana serikali ipo katika harakati za kuitafutia ufumbuzi," alisema Bw.Pinda.

Alisema serikali haikumyima mbunge huyo dhamana bali yeye mwenyemwe alikataa na kuamua kukaa mahabusu kwa sababu zake mwenyewe. "Tarehe 28 mwezi uliopita Lema na wenzake walikamatwa Arusha kwa madai ya kufanya maandamano bila kupewa kibali, tarehe 31 walipelekwa mahakamani,

kilichotokea wakati wa kupewa dhamana mbunge huyo kwa upande wake aliikataa na kudai anataka aendelee kukaa mahabusu,"alisema. Hata hivyo Bw. Pinda alisema kinachosubiriwa ni uamuzi wa Mahakama hapo Novemba 14, mwaka huu ili ifahamike kama ataendelea kukataa dhamana au atakubali.

No comments:

Post a Comment