11 November 2011

Waziri Mkuu Pinda apigilia msumari kwa Uingereza

Asema hata wanyama hawafanyiani ushoga

*Asisitiza hatutakubali vitendo vichafu
*Asema hata wanyama hawafanyiani ushoga

SAKATA la ushoga bado linafukuta nchini ambapo Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda amemtolea uvivu Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameroon kwa kauli yake ya kuzitaka Nchi za Afrika kukubali vitendo vya ushoga na kwamba, vitendo hivyo ni uchafu.

Hivi karibuni, Bw. Cameroon alitoa kauli ya utata akizitaka Nchi za Afrika kukubali vitendo vya ushoga na kwenda mbali zaidi kuwa, kama vitendo hivyo havitakubalika nchi yake itasitisha misaada kwa nchi hizo.

Waziri Pinda alisimamia msimamo wa serikali ambao ulitolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Benard Membe kuhusu tamko hilo na kusisitiza kuwa, taifa halipo tayari kuruhusu vitendo hivyo ambavyo vinakinzana na mila na desturi ya Mtanzania.

Akijibu swali la mbunge wa viti maalum Bi. Regia Mtema (CHADEMA) bungeni Dodoma jana kuhusu  msimamo wa serikali juu ya kauli ya Bw. Cameroon hasa kuhusu kutishia kufuta misaada kwa nchi zote ambazo hazitakubali kuunga mkono vitendo hivyo, Bw. Pinda alisema, Tanzania haipo tayari kuungana na kauli hiyo.

Bw. Pinda alisema, kuruhusu vitendo vya kishoga ni sawa na kumdhalilisha Mtanzania kwa kuwa, vitendo hivyo viko nje ya maadili na kuongeza kwamba, suala la ushoga ni hatari zaidi kwa kuwa, hata wanyama wasiokuwa na akili hawaendeani kinyume.

Akifafanua zaidi Bw. Pinda alisema kwamba, awali serikali ilionesha msimamo wake kwamba

haitakubali uchafu huo wala kuunga mkono.

"Mheshimiwa spika, Mheshimiwa Regia anataka kauli ya serikali juu ya kauli ya Bw. Cameroon, jambo la msingi hapa ni serikali inasema nini kuhusiana na kauli hiyo, lakini tayari serikali imeshaonesha msimamo wake kuhusiana na

jambo hilo kwamba haiwezi kuliuga mkono wala kulitambua.

"Kwa kuwa baada ya Waziri Membe kutoa kauli  ilikuwa ni kauli ya serikali, ninachosema hata wanyama hawafanyi hivyo. Mimi sikubaliani kabisa na uchafu huo," alisema Wazirui Pinda.

No comments:

Post a Comment