11 November 2011

Maandamano ya CHADEMA yamezorotesha umakini serikalini

Asema viongozi wamekuwa yakiyatafakari badala ya maendeleo

Na Godfrey Ismaely, Dodoma


WAZIRI Mkuu Bw. Mizengo Pinda, amesema maandamano ya mara kwa mara yanayaofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yameifikisha serikali katika hatua mbaya kwa kuwa inasababisha viongozi kukosa umakini wa kutafakari masuala ya maendeleo ya wananchi.



Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya serikali kusitisha maandamano ya
aina yoyote yanayofanywa na CHADEMA baada ya kuwepo kwa taarifa za kuzihusisha na uvunjifu wa amani.

Bw. Pinda aliyasema hayo jana Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali ya papo kwa papo iliyoulizwa na Mbunge wa Ubungo Bw. John Mnyika, (CHADEMA) katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Katika swali lake Bw. Mnyika aliyetaka kujua hatima ya mgogoro wa umeya katika Jiji la Arusha ambao umekuwa ukisababisha vurugu za mara kwa mara ikiwemo maandamano.

"Tusilikuze sana ili jambo mheshimiwa Mnyika hasa ile stahili yenu ya maandamano kila mahali," alisema.

Alisema suala la kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa umeya wa Jiji la Arusha bado linaendelea kwa kuwa awali alidhani mkakati wake wa kumuagiza msajili wa vyama vya siasa Bw.Jonh Tendwa, kulifanyia kazi lingefanikiwa lakini bado muafaka zaidi unaendelea kutafutwa.

"Sisi tuliopo serikalini stahili zenu za maandamano ya mara kwa mara tumekuwa tukishindwa kufanya kazi kwa umakini kwa ajili ya maendeleo ya wananchi;

"Tumekuwa tukiyafikiria maandamano kila siku, kwa kweli kwa hali hii mnapaswa kubadilika na kufikiria zaidi namna ambavyo tutawasaidia Watanzania badala ya maandamano tu kila siku,"alisema Bw. Pinda

No comments:

Post a Comment