Na Grace Ndossa
TAASISI ya utafiti ya utetezi wa haki za Aridhi imekabidhi hundi za sh. milioni tatu kwa waandishi wa habari watatu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina wa hali ya uwekezaji kwenye nishati mimea kwa lengo la kuibua masuala yaliyofichika na yanayoendelea kuathiri jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa haki ardhi Bw. Yefred Myenzi, alisema waandishi hao wataibua masuala mbali mbali ambayo yatakuwa kichocheo cha mijadala na maamuzi sahihi katika ngazi mbali mbali za utoaji maamuzi kuanzia vijijini hadi kwa watunga sera na sheria za ngazi za Taifa.
Alisema kuyaibua masuala hayo kutasaidia kujenga uelewa na uwezo wa jamii kutambua haki na wajibu wao, kudadisi na kuhoji maamuzi yasiyo zingatia maslahhi yao, kulinda rasilimali za Taifa zilizo katika maeneo yao, na kuchukua hatua juu ya uonevu, unyanyasaji, na ukiukwaji wa sheria na taratibu unaofanywa na wenye nafasi za kisiasa, na kiuchumi.
"Mchakato wa kuwapata washindi wa kuandika habari hizo tulitoa tangazo kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kualika waandishi kuwasilisha hoja za kiuchunguzi, ambapo jumla waandishi sita waliwasilisha maandiko yao na mchujo ulifanywa na kamati maalum ya programu kwa kuzingatia vigenzo vilivyowekwa,"alisema Myenzi.
Alisema kati ya waandishi sita waliyokidhi vigezo ni waandishi watatu ambao ni Mwandishi wa The guardian Bw. Gerald Kitabu, Mlimani TV Bw. Amin Mgheni, na mwandishi wa mwananchi Bw. Obeid Othman.
Naye Mwakilishi kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bw. John Mireny, kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bw. Kajubi Mukajanga, alisema waandishi hao wanatakiwa kufanya kazi kweli na si kukaa ofisini na kuandika.
Alisaema kumekuwapo na hitaji la kufanya uandishi wa kiuchunguzi katika maeneo mbali mbali nchini ili kuibua masuala yanayoigusa jamii ya wazalishaji wadogo.
Alito wito kwa waandishi hao waliopata hundi hizo kufanya habari za uchunguzi ambao utaibua mijadala mbali mbali katika jamii na si kuandika taarifa tu na kufika katika maeneo waliyoainisha.
No comments:
Post a Comment