Na Mwali Ibrahim
BAADA ya kushindwa kuitambulisha bendi ya Taarabu ya Mashauzi Classic Zanzibar kufuatia kutokea kwa ajali ya MV Spice sasa kundi hilo linatarajia kutambulishwa rasmi Novemba 12 katika ukumbi wa Magereza Zanzibar.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Zanzibar, Meneja wa ukumbi huo Rose Kikwa alisema utambulisho huo ulitakiwa kufanyika mwezi uliopita ambapo kwa bahati mbaya siku hiyo ndio ajali ya meli ilipotokea ivyo kuacha msiba huo upite na kujipanga upya.
Alisema, hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa kundi hilo kutoaburudani Zanzibar tangu kuanzishwa hivi karibuni hivyo utambulisho huo utakuwa ni maalum kwa wakazi wa huko kusikia nyimbo za kundi hilo kwa mara ya kwanza.
Rose alisema, kundi hilo linajumla ya nyimbo 11 ambazo zitatambulishwa siku hiyo huku kundi hilo likiongozwa na aliyekuwa muimbaji wa Jahazi Aisha Ramadhani 'Isha Mashauzi'.
Kundi hilo tayari limekamilisha Album mbili, Album ya kwanza ikiwa na nyimbo nne ambazo ni nani kama mama ambayo imebeba jina la Album, baraka za baba, Mamaa Mashauzi mtoto kutoka Musoma na Umdhaniaye ndiye kumbe siyo .
Nyingine inajumla ya nyimbo tano ambazo ni Hakuna kati yenu wa kunirusha roho, La mungu halina muamuzi, Niacheni nimpende, Sitosahau kwa yaliyonikuta na anayejishuku hajiamini.
No comments:
Post a Comment