Na mwali Ibrahim
KOCHA wa timu ya taifa ya gofu, Farayi Chitengwa ametangaza rasmi kikosi cha wachezaji 8 wanaounda timu ya taifa ya mchezo huo watakaowakilisha katika mashindano ya Challenge afrika Mashariki ya gofu yanayotarajia kufanyika Novemba 8 hadi 11, kwenye viwanja vya Klabu ya Gymkhana Arusha.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Arusha jana, Chitengwa alisema timu inaendea na maandalizi kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yatashirikisha nchi za Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na wenyeji Tanzania.
Aliwataja waliochaguliwa kuunda timu ya taifa ni nahodha Frank Roman, Adam Abass kutoka Klabu ya Gymkhana Moshi, John Leons, John Saidi, Elisante Lembris, Nuru Mollel (Gymkhana Arusha), Aidan Nziku na chipukizi Victor Joseph kutoka Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.
Chitengwa alisema Jimmy Mollel atakuwa mchezaji wa akiba kwenye timu ambapo wachezaji hao walipatikana kupitia mashindano ya Dar open yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya gofu vya Lugalo ambapo jumla ya wachezaji 100 walichuana.
"Tumechagua wachezaji wenye uwezo mkubwa na sasa wanaendelea na mazoezi na imani wataweza kuwakilisha nchi vyema katika mashindanho hayo na kuchukua ubingwa tukiwa kama wenyeji," alisema Chitengwa.
No comments:
Post a Comment