03 November 2011

Mabondia watishia kutopanda ulingoni

Na Mwali Ibrahim

MABONDIA Francis Cheka na Kalama Nyilawila wamesema wanahatihati yakutopanda ulingoni Desemba 31 kufuatia promota wa pambano lao kushindwa kuwalipa pesa kwa ajili ya kucheza pambano hilo.
Pambano hilo lisilo la ubingwa la uzito wa kg 76 lilitarajiwa kufanyika katika uwanja wa jamuhuri mkoani morogoro.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nyilawila alisema, promota huyp philimon Kiyando ameshindwa kuwalipa pesa hadi sasa kwa ajili ya pambano hilo ambapo aliwapa pesa kidogo kwa ajili ya mazeozi.

"Siku zinakaribia anatakiwa atulipe pesa ambazo tunamdai kiasi cha sh. Milioni mbili kila mmoja lakini amekuwa akituzungusha sasa sisi tumeamua kutokuendelea nae kwa sasa tumeamua kumtafuta promota mwingine kwa ajili ya kutuandalia pambano," alisema Nyilawila.

Alisema, watakaa na vyama vya ngumi za kulipwa ambavyo ni PST na TPBC ambao ndio wanawasimamia kwa ajili ya kuzungumza nao kuhusiana na hilo swala na kujipanga upya.

Naye kwa upande wake Cheka alisema promota anaonekana ni mbabaishaji hivyo hawataweza kuendelea naye kwani kutrokuwapa pesa zao ni kuonekana kabisa ameshindwa kumudu maandalizi ya pambano kwani aliishia kuwapa pesa za mazoezi na bado ni kidogo.

"Anatupotezea tu muda wetu na kutukosesha kupata mapambano kutokan ana pambano lake hili tumekuwa tukimpigia simu ili kujua hatima ya pambano lakini amekuwa akituzungusha mara nipo huku au ntawapigia baadae tayari tumeisha muona hatufai," alisema Cheka.

Lakini baada ya kutafutwa promota huyo kwa kupitia simu yake ya kiganjani simu ili kuwa haipatikani kila ilipo pigwa kwa ajili ya kumtaka kuzungumzia hilo swala.

No comments:

Post a Comment