*Polisi Arusha yaingia tuhuma nzito
JESHI la Polisi Mkoani arusha linadaiwa kuingia katika kashfa nzito baada kumshikilia mwekezaji wa kigeni kutoka nchini Italia, Bw. Patricio Icioni, na kumuacha huru katika mazingira ya kutatanisha wakati akiwa anatuhumiwa kuiba ngozi zenye thamani ya sh. milioni 520.
Bw. Icioni pamoja na wenzake wanne akiwemo, Bw.Jamal Abdulwadood ambaye naye anadaiwa kutafutwa na jeshi hilo kwa muda mrefu wanatuhumiwa kuhusika na wizi wa ngozi za mbuzi,ng'ombe na kondoo zenye thamani ya dola za kimarekani 324,402.00 ambazo ni zaidi ya sh. milioni 520 mali ya kampuni ya Salex Limited ya mkoani humo.
Jeshi hilo linadaiwa kuingia katika kashfa hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kumtorosha mwekezaji huyo Juni mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha huku wahika wake wakishindwa kutoa ufafanuzi juu ya sakata hilo.
Inadaiwa kuwa wahusika wa jeshi hilo wanashindwa kutoa ushiriakino kuhusu suala hilo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni hofu ya kushughulikiwa na wakubwa wao iwapo watatoa taarifa itakayoleta mkanganyiko.
Wengine waliohusika katika sakata hilo ni raia wa Kenya, Bw. Obara Vitalus, Bw. Ally Saad Baasabra na Mtanzania, Bw. Victor Charles ambao tayari wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mkoani humo mbelea ya Hakimu Bw. Charles Magesa ambapo watuhumiwa wawili waliunganishwa na, Bw. Vitalus Agosti mwaka huu.
Uchunguzi wa mwandishi wetu umebaini kuwa, Bw.Icioni alikamatwa na Jeshi hilo kwa jitihada za wasamaria wema baada ya kutafutwa kwa muda mrefu mjini Morogoro kati ya mwezi Machi na Aprili mwaka huu na kuachiwa kwa dhamana kwa madai ya kutoa nafasi ya kufanywa kwa uchunguzi wa tuhuma hizo kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa.
Ilidaiwa kuwa licha ya dhamana kuwa ni haki kwa kila mtu kulingana na sheri za nchi lakini wakati mtuhumiwa huyo anaachiwa jeshi hilo halikuzuia hati ya yake ya kusafiria baada ya kudhaminiwa na jamaa yake aliyetajwa kwa jina la, Bw.Ally Mohammed Akrab mkazi wa Arusha.
Pia jeshi hilo linadaiwa kukalia jalada la mtuhumiwa huyo pamoja na watuhumiwa wengine katika shauri hilo bila kulikipeleka kwa Mwendesha Mashitaka ili kufikishwa mahakamani kwa lugha iliyozoeleka ya 'upelelezi bado unaendelea' huku ikidaiwa kuwepo kwa mbinu za kutaka kuvuga kesi hiyo.
Habari zaidi zimebaini kuwa baada ya jalada hilo kurudi Polisi kutoka kwa
mwanasheria wa serikali mwezi Juni mwaka huu, watuhumiwa hao walitakiwa
kurudi Polisi tayari kufikishwa mahakamani, lakini katika hali ya
kushangaza mtuhumiwa Icioni licha ya kuwepo Polisi siku hiyo walishindwa kumfikisha mahakamani.
Inadaiwa kuwepo kwa mvutano wa ndani kwa ndani kwa jeshi hilo kuhusu mpango wa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao kipindi hicho baada kuwepo kwa nguvu kubwa ya kutaka Bw.Icioni, asifikishwe mahakamani mpango unaodaiwa kufanikiwa baada ya watuhumiwa wengine kufikishwa huku yeye akiachiwa kwa dhamana katika mazingira tata.
Shauri hilo lilipotajwa Agosti mwaka huu Bw.Icioni na, Bw. Jamal hawakutokea
mahakamani huku Wakili anayewatetea, Bw. Method Kimomogolo, akiiomba mahakama hiyo kuwapa muda zaidi wateja wake ili waweze kufika tarehe
iliyopendekezwa.
hata hivyo tangu wakati huo hakuna aliyefika mahakamani licha
ya mahakama hiyo kutoa hati za kuitwa na kukamatwa mara kadhaa lakini hakuna kilichofanyika.
Awali Mahakama hiyo ilitoa hati ya kuitwa mahakamani kwa raia hao wa
kigeni lakini mara ya pili ilitoa hati ya kukamatwa kwa Patricio huku
ikiendelea kulisihi jeshi la Polisi kumsaka na kumleta Bw. Jamal maagizo ambayo hayakutekelezwa.
Kutokana na hali hiyo Mwendesha mashitaka wa serikali Bi. Ellen Mwijage, aliomba mahakama kutoa hati nyingine ya kumkamata kwa mtuhumiwa huyo.
Hata hivyo, Novemba 2, mwaka huu hakimu wa mahakama hiyo, Bw. Magesa alizidi kusisitiza kukamatwa na kuletwa mahakamani hapo kwa raia hao wawili wa kigeni,Patricio na Jamal ili kuunganishwa na wenzao katika kesi wanaoyotuhumiwa nayo ya wizi wa ngozi.
Kutolewa kwa hati ya kukamatwa kwa raia huyo wa Italia, na hati ya kuitwa
kwa Mkenya kunafuatia polisi kushindwa kuwafikisha watuhumiwa hao
mahakamani kwa muda mrefu pamoja na kutolewa kwa hati ya kukamatwa na za
kuwaita ili waunganishwe na wenzao watatu katika kesi hiyo.
Bw. Magesa alisema kwa kuzingatia kumbukumbu za kesi hiyo, watuhumiwa
waliitwa kujibu mashitaka yanayowakabili Agosti,17 mwaka huu, lakini
Septemba 2, mwaka huu wakili wao, Bw. Kimomogolo aliiambia mahakama hiyo kwamba atahakikisha watuhumiwa hao wanafika jambo ambalo halijatekelezwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Bw. Akili Mpwapwa, alipotakiwa
kuzungumzia tuhuma hizo alisema jitihada za kumsaka mtuhumiwa huyo
zinaendelea na kueleza kuwa kumsaka mtuhumiwa hakuna muda maalumu hivyo
wanahitaji muda zaidi katika kuwatafuta.
Alipoulizwa sababu za mdhamini wa, Bw. Patricio kutokamatwa kama inavyofanyikwa kwa watu wengine watuhumiwa wanapokosekana mahakamani Kamanda Mpwapwa alisukuma lawama kwa Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa Arusha (RCO) kuwa ndiye anayeweza kujibu vizuri swali hilo.
“Haya mambo siyafahamu vizuri, RCO ataelezea vizuri zaidi, lakini kwa
ujumla linashughulikiwa na litafikia mwisho japo mahakama ndiyo yenye
mamlaka ya kutoa maelekezo na sisi niwatekelezaji tu,”alisema Kamanda huyo
bila kufafanua zaidi.
Tanzania hatuna Jeshi ndugu zangu!
ReplyDeleteNchi nyingine huwezi kuwa polisi bila degree sisi mtu anakuwa polisi ikiwa kama ana uwezo wa kuwarushia makombora wananchi kwenye maandamano. Waulize maposi wetu wangapi wanaofahamu haki za binadaamu na ulinzi wa taifa na mali zake?jibu ni wachache sana.
Anganlieni kigoma yaliyotokea, ni kunaonesha kuwa jeshi letu na ulinzi wa taifa ni duni sana. Wanasema mipaka mikubwa mbona miaka ya sabini walowezi walikamatwa within five minutes siku hizi majasusi wanaishi tanzania miaka tele bila shida.
Sijui kitatokea nini next..... sijui hata kama makombora yaliyochakaa yamefanyiwa kazi au tusubiri kifo tena..... Usafiri mbaya, umeme hamna na wezi wa rushwa na mali zetu wanaongezeka.
shida!