07 November 2011

Kozi ukocha Daraja C kuanza leo

KOZI  ya Ukocha kwa ajili ya kupata leseni za Daraja C kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), itafanyika leo katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema jumla ya makocha 30 ndiyo wanaoshiriki kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi wanne akiwemo Kocha Mkuu wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Jan Poulsen kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Wakufunzi wengine ni Kasimawo Laloko (Nigeria) na Sunday Kayuni wanaotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) na Kim Poulsen kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU).

Wambura aliwataja  washiriki wa kozi hiyo kuwa ni Abdul Nyumba, Absolom Mwakyonde, Ahmed Mumba, Christopher Eliakim, Dismas Haonga, Edward Hiza, Eliasa Thabit, Emmanuel Massawe, Fulgence Novatus, Gabriel Gunda, Gideon Kolongo, Haji Amir na Hassan Banyai.

Wengine ni Juma Mgunda, Jumanne Ntambi, Keneth Mkapa, Leonard Jima,  Maarufu Yassin, Maka Mwalwisi, Mecky Maxime, Mohamed Tajdin, Mussa Furutuni, Mussa Kamtande, Peter Mhina, Richard Kabudi, Sebastian Nkoma,  Stephen Matata, Tiba Mlesa, Wane Mkisi na Wilfred Kidau.

Wambura alisema kozi hiyo itafikia tamati Novemba 20, mwaka huu na wahitimu watakabidhiwa vyeti vya uhitimu wa kozi hiyo.

No comments:

Post a Comment