10 November 2011

RAIS Jakaya Kikwete - Mgeni Rasmi TPN

Na Flora Amon.

RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la kihistoria litakalowakutanisha  wanataaluma nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Rais wa mtandao wa wanataaluma  nchini (TPN) Bw.Phares Magesa alisema  kuwa kongamano hilo litafanyika Desemba 4 mwaka huu katika ukumbi la Mlimani City ikiwa ni sehemu yakushereke miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara.

Alisema kuwa dhumuni la kongamano hilo ni kuimarisha uwezo na wajibu wa wanataaluma kuendeleza jamii ya Tanzania na kushawishi maamuzi katika ngazi mbalimbali katika sekta za umma na selta binafsi kwakutoa hoja madhubuti kitaaluma na maarifa.

Alisema kuwa,hao kama wadau muhimu katika maendeleo ya Tanzania,ambapo tangu kuanzishwa kwake kumekuwa wakihamasisha wanataaluma wa kitanzania kuungana katika kushiriki katika maamuzi,kuunga mkono na kuteleza sea nzuri,huku wakihakikisha wanawasaidia watanzania wengine katika maendeleo yao ya kijamii na kiuchumi.

Alisema kuwa TPN imeamua kuitisha kongamano la wanataaluma ili kujadili mafanikio na changamoto za Tanzania tangu uhuru na kuchambua majukumu yaliyotekelezwa na wanataaluma katika safari ndefu .

Alisema kuwa mambo yatakayoimizwa kwenye kongamano hilo yatakuwa mwongozo kwa mipango ya mtandao huo kusonga mbele.

"Kongamano hili litawashirikisha wanataaluma mbalimbali,watunga sera,wanasiasa na wawekezaji wa viwanda kwa nia ya kujadiliana juu ya majukumu yao ya pamoja kwa njia ya kukosoana kwa njia ya majadiliano yenye kujenga nchi"Bw.Magesa.

Pia wataaluma hao watachambua jinsi wataaluma walivyofanya au ambavyo walipaswa kufanya katika miaka 50 ilipita  ikiwa pamoja na kuchambua iwapo sera za sasa na mifumo ya nchi vinaweza kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati,kikitilia maanani mpango wa Mkukuta na diya ya maendeleo kufikia mwaka 2025.

Aidha wanataaluma watachambua mfumo wa elimu nchini na kuangalia iwapo una ubora wa kuendeleza nchi , juu ya taaluma na maadili na kuimarisha uhusiano wa tanzania na wataaluma wanaoishi Tanzania.

Siku ya kongamano hilo kutakuwepo wachokoza mada mabalimbali  na watawasilisha masuala ya kimkakati katika kuendeleza nchi.

No comments:

Post a Comment