10 November 2011

Nyilawila: Don King ananipa ugumu

Na Mwali Ibrahim

BONDIA Karama Nyilawila, amesema kutopata mawasiliano na promota wa pambano lake, Philemon Kyando 'Don King' dhidi ya Francis Cheka kunampa wakati mgumu kujiweka sawa kufanikisha dhamira yake ya kuongeza uzito.

Nyilawila alikuwa na uzito wa kg. 72 lakini alijipanga kutumia pambano hilo kuongeza hadi kg. 76, ili kumfikia Cheka kwa ajili ya kupambana.


Pambano hilo lilipangwa kufanyika Desemba 31, mwaka huu katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro likiwa la raundi 10 lisilo la ubingwa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Nyilawila alisema, kinachomsumbua ni mkataba waliousaini ambao tayari wamechukua fedha za utangulizi, ambapo kila mmoja wanamdai Don King sh. milioni tatu ambazo walikubaliana.

Hata hivyo Nyilawila alisema, aliamua kumtafuta promota mwingine kusimamia pambano, hilo lakini anashindwa kufanya hivyo kwa kuwa tayari wamesaini mkataba na Don King, kitu ambacho kinaleta ugumu.

"Sijui hatima ya pambano letu hadi sasa, kwani kwa sasa promota ndiye hapatikani hata katika simu yake ya mkononi pia kibaya zaidi tuna mkataba naye, kitu ambacho kinanikwamisha kujiandaa vyema.na tayari tumeisha sainiana kataba sasa mimi inanikwamisha kwani," alisema Nyilawila.

Alisema yyupo tayari kucheza siku yoyote atayakayopanga promota, lakini anatakiwa kuwajulisha kama analisogeza ama lipo kama ilivyopangwa awali ili waweze kujiandaa vyema.

Lakini alisema, bado anaendelea na mazoezi kwa kuwa hawezi kuacha akiwa kujiandaa.

Promota huyo alipopigiwa simu yake ya mkononi kuzungumzia pambalo hilo, hakuweza kupatikana kwani simu yake ilikuwa haipatikani.

No comments:

Post a Comment