03 November 2011

Muswada wa katiba urudishwe kwa wananchi kwanza-Wanaharakati

Na Rehema Maigala

WANAHARAKATI wa Baraza la Katiba Tanzania wamesema muswada utakaowasilishwa bungeni usomwe kwa mara ya kwanza ili kuwapa fursa mwananchi kutoa maoni yao kama katiba ya sasa inavyoelekeza.


Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa jukwaa la Katiba Tanzania Bw. Deus Kibamba, alisema iwapo muswada huo utasomwa kwa mara ya pili na tatu utakuwa ni upotoshaji kwa kuwa wananchi hawatakuwa na fursa ya kutoa maoni yao.

"Muswada huu ni mpya hivyo inatakiwa itambulike kuwa ndio unasomwa kwa mara ya kwanza, ule uliosomwa bungeni kwa mara ya kwanza mwezi Aprili haukuleta mafanikio na kwa sasa hauwezi kuletwa kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya pili kana kwamba ulisomwa kwa mafanikio,"alisema Bw. Kibamba. 

Alisema kukataliwa kwa muswada huo kwa mara ya kwanza ni dhahiri kuwa yapo  baadhi ya mambo ambayo yameweza kubadilika kulingana na maoni ya wasomi, wataalam na wananchi juu ya muswada huo.

Hata hivyo alisema imeoneka kuwa kuna kusuasua katika kukamilisha muswada huo kwa ajili ya kuwasilisha bungeni na kwamba ulitakiwa kuwasilishwa mpya katika mkutano wa bajeti uliokamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Alisema katika awamu hii muswada huo umeshereweshwa kuchapishwa katika gazeti la serikali na kunyima fursa wananchi kuuona, kuuchambua na kuujadili kabla ya kwenda bungeni.

Alisema katika mikutano yao ya pamoja na makongamano na semina na wananchi, walipendekeza kuwa muswada mpya ujadiliwe katika kila mkoa kuwe na kituo cha kujadili huo muswada.

Alitaja vipengele ambavyo vinaonyesha serikali kukosa umakini katika kuandaa muswada huo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa bunge maalumu la katiba yenye  wajumbe wanaojumuisha wabunge wote na wawakilishi wote wa baraza la wawakilishi kutoka Tanzania Visiwani.

Naye Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake (TAMWA) Bi.Ananilea Nkya, alisema kutolewe muda wa kutosha kwa wananchi kupata muswada na kujadili kabla ya kuwasilishwa kwa majadiliano rasmi bungeni.

Kwa mujibu wa serikali baada ya bunge kujadili na kupitisha muswada huo wa sheria tume maalum itaundwa na Rais Kikwete kwa kushauri na Rais wa Tanzania Visiwani na Mwansheria Mkuu wa serikali. Tume hiyo inatarajiwa kujumuisha makundi yote ya jamii.

Tume hiyo ndiyo itayotembea nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya wanayoitaka. Kazi ya uundwaji Katiba Mpya unatarajiwa kukamika mwaka 2014 hku vipengele vinavyoonekana kuwekewa mkazo zaidi ni madaraka ya Rais na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

3 comments:

  1. WANAHARAKATI NA WATNZANIA WOTE MNAOITAKIA MEMA TANZANIA TUSIPOSIMAMA KIDETE HAKUNA KATIBA MPYA, CCM MAFISADI,WEZI HII KATIBA YA ZAMANI WANA MASLAHI NAYO, COZ INAWALINDA, WANACHAKACHUA CHAGUZI, RAIS NA MWENYEKITI WAO ANAKUWA MUNGU MTU, INABIDI TUWAFOSI KWA GHARAMA YOYOTE, KATIBA MPYA NDIO MWAROABAINI WA UTAWALA BORA NA CHAGUZI HURU NA ZA HAKI. SHIME WATZ

    ReplyDelete
  2. CCM HAWAWEZI KUITOA KATIBA MPYA KWA HIARI, KWANI NDIO ITAKUWA MWANZO WA MWISHO WAO, CCM BILA KUCHAKACHUA HAISHINDI CHAGUZI, NA KTIBA MPYA ITALETA TUME HURU YA UCHAGUZI, MNAFIKIRI CCM WATATOA KATIBA MPYA KIRAHISI, VIONGOZI KARIBU WOTE MAFISADI, NA HII KATIBA NDIO KICHAKA CHAO KWA KUMRUNDIKIA RAIS MADARAKA NA WANALINDANA, DR SLAA NA WANAHARAKATI MTUONGOZE KUIPATA KATIBA MPYA WATZ TUPO NYUMA YENU.

    ReplyDelete
  3. Hapa sasa naona kuna Wajasilia mali wamejiaanda kutengeneza fedha katika hili la katiba. Hivi mwananchi wa Ifiga, Likawage, Ilolangulu, Ngorongoro au nanguruwe ataanza kufundishwa maana ya muswada au atajadili bili ya kujua.

    Kweli tumezoea watu kufikiri kwa niaba yetu maana tunataka katiba lakini bado TUNAPIGA RAMLI TU.

    Hawa wanaharakati ni Fedha oriented tukiwasikiliza Hawa hapa hakuna katiba mpya.

    Wanaharakati hii si Project nzuri kwenu mnatuchelewesha tafuteni viable projects tengenezeni proposals nzuri ili
    mtengeneze fedha.

    Wanaharakati (wajasili mali) msitake kuchezea mustakibali wanchi kwa dhamani chache Tunataka kusonga mbele kwenye JAMBO HILI LA KATIBA KAFANYENI MAMBO MENGINE

    Tanzanians let be vigilant these wanaharakati are looking at KATIBA issue as a source of making money. While wengine we are looking at it as the opportunity of remaping and redesigning the mustakibali wa nchi yetu for many years to come

    ReplyDelete