03 November 2011

Manispaa ya Kinondoni na changamoto ya biashara ndogo ndogo

Na Agnes Mwaijega

MANISPAA ya Kinondoni imesema mkakati wakuhakikisha  wafanyabiashara wanaopanga biashara zao barabarani na katika maeneo mengine yasiyo rasmi wanaondoka na kwenda katika maeneo rasmi ni changamoto kubwa ambayo inaikabili manispaa hiyo.
Pia imesema  mkakati wa kuhakikisha wafabiabiashara wote wanaondoka na kwenda katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya biashara itachukua muda mrefu kukamilika.

Akizungumza na majira Dar es Salaama jana Afisa Hsabari wa manispaa hiyo Bw.Sebastian Mhoela alisema sababu ya mkakati huo kuchukua muda ni ni ongezeko la wafanyabiashara kutoka katika mikoa mbalimbali.

Alisema pamoja na kwamba hiyo ni changamoto kubwa kwa manispaa hiyo ,itahakikisha wafanyabiashara hao wanaondoka katika maeneo yote yasiyo rasmi ili kupunguza kero.
"Mkakati huu wa kuwaondoa hawa wafanyabiashara unaanza rasmi lakini uekelezaji wake utachukua muda kukamilika kutokana na ukweli kwamba karibu kila siku wafanyabiashara wanaongezeka,"alisema.

Alipohojiwa kama manispaa hiyo imeshawapatia maeneo ya kufanyia biashra Bw.Mhoela alisema manispaa hiyo tayari imeshatenga maeneo kwa ajili ya wafanyabishara hao ambayo ni pamoja na Tegeta,Magomeni Ubungo na Manzese.

Alisema lengo la mkakati wa manispaa hiyo ni kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafanyia biashara zao katika maeneo rasmi ambayo yametengwa na serikali.

Aliongeza kuwa hiyo itasaidia kupunguza kero kwa wananchi kwa sababu wafanyabiashara wengi wanapanga biashara zao barabarani na katika maeneo mengine ambayo sio rasmi.

No comments:

Post a Comment