14 November 2011

Mchakato wa katiba mpya

Na Rachel Balama

MCHAKATO  wa uundaji wa katika mpya ni kiini macho kilichowekwa na serikali kwa nia ya kuwahadaa wananchi wakati serikali haina nia ya kufanya hivyo.

Kadharika serikali imetakiwa kuweka wazi kama kweli ina lengo la kuundwa kwa katiba mpya au kuifanyia marekebisho katiba ya sasa.


"Mimi binafsi naona kwamba serikali haina nia ya kuundwa kwa katiba mpya isipokuwa ina lengo la kuifanyia marekebisho katiba ya sasa ila wanatuadaha tu wananchi," alisema.

Kauli hiyo ilitolewa  Dar es salaam jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha National Reconstruction Alliance(NRA) Bw. Hassan Kisabya, wakati alipokuwa akichangia mada kwenye  mdahalo kuhusu muswada wa mabadiliko ya katiba.

Bw. Kisabya, alisema kuwa serikali haina nia ya dhati ya kuundwa kwa katiba mpya na badala yake kinachofanyika ni kiini macho tu.

Alisema kuwa hali inayoonyesha sasa ni kwamba serikali ina lengo tu la kufanya marekebisho kwenye katika ya sasa lakini si  kuunda katiba mpya.

Alisema katika kifungu cha 27 cha muswada wa mabadiliko ya katiba kinatoa jukumu kwa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania Bara(NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC)  kusimamia taratibu zote bara baada ya kutungwa kwa katiba na kupitishwa na bunge la katiba.

Alisema kuwa na katika kifungu cha 32 (3) mara baada ya katiba mpya kutungwa NEC na ZEC zitasimamia mchakato wa upigaji wa kura za ndio au hapana.

Alisema kuwa mara baada ya katiba kukamilika ndipo katiba zote mbili yaani ya sasa na itakayoundwa zitapigiwa kura za ndio au hapana na wananchi ambapo jukumu hilo litasiwamiwa na tume zote mbili za uchaguzi ambazo si huru.

Aliongeza kifungu hicho  cha 32 kigodo cha nne kinatoa mwanya pia kama kura za ndio
zitakuwa nyingi kuzidi kura za hapana basi itaendelea kutumika kwa katiba ya sasa jambo ambalo amedai si sahihi hata kidogo.

Haiwezekani rais ateue NEC na ZEC kuratibu na kutoa matokeo ya kura za ndio au hapana kwani tume hizo zinaweza kwenda kinyume na matokeo ya wananchi katika upigaji wa kura.

Alisema kuwa wananchi wanaweza kupiga kula za hapana nyingi lakini tume ikatoa majibu ya  tume ya kusimamia maikafanya kinyume cha hapo.

Bw. Kisabya, alitoa mapendekezo kwamba hakuna haja ya muswada huo ambao utapelekwa bungeni wiki ijayo kusomwa kwa mara ya pili badala yake usomwe kwa mara ya kwanza.

Aliwaomba wabunge bila kujali itikadi za vyama vyao kuhakikisha kuwa wanaupinga vikali muswada huo ili mchakato uanze upya kwa kuwashirikisha wananchi ili wapate fursa ya kuachangia kuanzia mwazo hadi katiba itakapokamilika.

1 comment:

  1. Bunge la Tanzania halina Spika bali kuna mwanamama kakaa pale mbele akiitetea serikali ktk ukandamizaji. Shime watanzania 2015 fanyeni kweli kuwaonyesha kuwa ss ndio tuliowaajiri na kututetea sio kuangalia maslahi binafsi na ya kichama. Sitta was the right person on that sit, not this madame makinda who does know how to describes things in the parliament.

    ReplyDelete