14 November 2011

Nape atamba kuyavua magamba yaliyokwama

Na Rachel Balama

KATIBU wa Uenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Bw. Nape Nnauye, amesema kuwa viongozi wote wanaojitapa  kwamba magamba yao yapo kiunoni na hayawezi kuondolewa wanajidanganya,  yataondolewa kwa shoka kwenye kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.


Bw, Nauye, alitoa kauli hiyo Dar es salaam jana wakati alipokuwa akizindua tawi la CCM barabara ya Pamba.

Alisema kuwa wakati huu CCM inapoendelea na kampeni yake ya kujivua gamba kuna baadhi ya viongozi ndani ya chama na serikali wanadai kwamba magamba yao hayawezi kutoka kwa kuwa yapo kiunoni si kweli na yatatoka tu.

"Wale ambao magamba yao yapo kiunoni na hayawezi kuondolewa tutatumia shoka kuyaondoa katika kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa", alisema.

Alisema kuwa kuna baadhi ya viongozi wanatumia ilani ya CCM kwa ajili ya kunufaisha matumbo yao hali inayopelekea wananchi kupoteza imani na chama pamoja na serikali.

Alisema kuwa atapambana na mafisadi hadi kieleweke ili kila mwananchi wa tanzania aishi maisha bora na kamwe hatomuogopa mtu yoyote  wakati akipigania usawa kwa wananchi wote.

Alisema kuwa kama aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya awamu ya kwanza hayati Edward Sokoine alichukiwa na baadhi ya watu haijalishi yeye akichukiwa pia kwa kutetea maslahi ya wananchi.

"Alichukiwa hayati Sokoine itakuwa mimi, mimi ni zaidi ya Babu wa Loliondo nitawashughulikia tu mafisadi ili kila mtu ajifunie kuwa mwana CCM," alisema.

Alisema kuwa leo viongozi wengi wamekuwa matajiri kupita kiasi huku wananchi wengine wakiendelea kuwa masikini kutokana na ufisadi.

Alisema kwamba kamwe hawezi kunyamaza hadi pale atakapoona nchi inatawalika kwa usawa.

Alisema kuwa atapambana vikali ili kuhakikisha kwamba tofauti ya vipato kati ya walionacho na wasionacho haitofautiani sana ili wananchi waweze kujenga imani na chama.

Pia Bw. Nnaye aliwataka vijana wa CCM kupambana kwa lengo la kuwashughulikia wale wote wanaofanya dhuruma kwa kuwadhurumu watu kwa namna moja ama nyingine.

Bw. Nnauye, aliwataka watu wote watakaodhurumiwa  serikalini kukimbilia kwenye tawi hilo la Pamba na kama itashindikana basi waende kwake na atapambana na wadhurumaji hao hadi kieleweke.

"Wananchi wengi wamekuwa wakidhurumia mali zao kama ardhi na vitu vingine , sasa nasema waje kwangu nitapambana na wadhurumaji," alisema.

Aisha

Katika hatua nyingine Bw. Nnauye, alisema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) sasa kinakuwa ni chama cha kigaidi na si cha siasa.

Alisema kuwa chama chochote cha siasa hakiwezi kufanya matendo ya kigaidi kama kinavyofanya chama hicho.

Alisema Bw. Lwakatare ambaye aliwahi kuwa CUF sasa amepeleka vurugu zote CHADEMA.

"Bw.Lwakatare alipokuwa CUF chama kilikuwa na vurugu kubwa sasa ameziamishia vurugu zote za kigaidi CHADEMA," alisema.

Bw. Nnauye alisema kuwa wana uwezo wa kuwashughulikia watu wote wanaofanya vurugu na kuwataka wananchi kujiepusha na chama hicho kwa kuwa kinawapeleka sehemu siko.

Aliyataka matawi yote ya CCM nchini kutoshughulika na siasa pekee na badala yake pia yawe ni sehemu ya uzalishaji kwa lengo la kujiongezea kipato na kupambana na umasikini.

Katika uzinduzi huo Bw.Nnauye aliwataka wanachama wa tawi hilo kuanzisha mfuko wa tawi ambapo aliahidi kutoa sh. milioni mbili.

11 comments:

  1. unaanzisha malumbano mapya nape tumia hekima ktk maneno yako ya kuwaita wenzio magaidi maana na wao wakianzaa kuiita ccm magaidi tutaharibu mipango ya maendeleo na itakua kushutumiana sasa huyu gaidi na yeye aakisema huyu gaidi pia. tushughulike maswala ya msingi ktk chama chetu ccm.epuka kuanzisha somo jipya ambalo lilikua halipo. yapo mazuri na mabaya kwa kila upande lkn tuangalie namna ya kuweka hali shwari na nchi itawalike kama ulivyosema. sikuzote kibaya cha jitembeza na kizuri chajiuza nadhani wanaanchi ni waamuzi wa hayo na sio sisa za kupakana matope tushughulikie mambo ya msingi kma kuondoa dhuluma,ufisadi,rushwa, maendeleo,nakadhalika vitu amabavyo vinamkera kila mwananchi nadhani hapo ndo tutakua tumetimiza wajibu. asanteni wapenda maendeleo na haki!

    ReplyDelete
  2. Anayejaribu kuendeleza mchezo wa kuvuviziana na unayemvizia umemuacha akajua unachofanya akikurudi shaurilo. Tatizo kubwa ni kutojua kuwa hujui kuwa hufahamu na utakapojua utakuwa umechelewa sana.

    ReplyDelete
  3. nyinyi ni wasaniii tu, maisha bora yako wapi ! musitufanye kama wote wajinga ! chama mumekiua na serikali nayo mumeivuruga !kujivua gamba imekuwa wimbo wa taifa ? ccm na serikali yenu mumejaa malumbano,makundi,masengenyo,matusi,ushabiki na kejeli tu !you guys mumepwaya sanaa, si ndani ya ccm wala serikalini ! trust me, hamutaweza kukwepa the winds of changes ! its just the matter of time ! wananchi siku hizi wana akili ati !

    ReplyDelete
  4. CCM nyenyewe ni gamba katika nchi yetu, je wananchi wachukue shoka kujivua na hiki chama. Makada , tafadhali msitumie maneno yanayoweza kuhatarisha amani nchini. Hakuna mwanachama msafi CCM. Mnajidanganya wenyewe.

    ReplyDelete
  5. nape maneno matupu vitendo hakuna,kuwa kama mrema back in the days kabla ccm haijamvika gamba

    ReplyDelete
  6. NNAPE!!! yupi gaidi kati anayewaongoza wananchi kuzifahamu na kuzidai haki zao? na anaye wapiga risasi za moto wananchi wake kwa kudai haki zao? Nawaomba mruke rukeeee na mshike kila mti unaoweza wasaidia..... Ila mkae mkielewa haki ya mtu haidhulumiwi....Zambia ni mfano mzuri....Mbeya yaliyotokea msifanye hamyoni.....Nawaomba mkae kimya tuu Nchi hii haikuumbwa kwa maufaa ya kikundi cha watu... Ni yetu sote na hakuna mwenye hati miliki na TANZANIA.......Kimya kingi kina mshindo.....Siamini kama Tutafika huko anakokusema CHAWENE,simba kama CHAMA na SERIKALI ikifahamu UPINZANI si UADUI ila NICHAGIZO KATIKA KUTEKELEZA ILANI YA CHAMA....MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  7. Mnh Nape unatisha,
    Chadema chama cha kigaidi CCM, Serikali na vyombo vyake vya dola mpo na hamjamkamata hata mmoja kwa ugaidi. Rwakatare gaidi mnapishana naye au yuko kwenye mtaro? kazi ya propaganda ndio hiyo, mbichi kuita mbivu na spade kuita kijiko.
    hakuna gamba na ngozi ndani ya ccm hapo ni kulindana tu. nakuamini una nia njema na nnji hii muda mrefu kama mrema lakini lakini strategy zako na maneno unayotumia havijaenda shule

    ReplyDelete
  8. nape watanzania si mbumbumbu tena, wala zidumu fikira za ccm au za mwenyekiti haikubaliki
    Tukiandamana chadema, tukidai mkopo wa masomo chadema, sisi hatufikiri? tukiomba mjadala wa wazi wa katiba chadema. nadhani hata ukiota jinamizi siku hizi unamwona slaa mbowe na watu wake pole. ati wanava magwada waangalie UVCCM wanavyovaa kwa asili yao. unajua TYL ya nyerere? kwani chadema ni nani au ndio unawaita magaidi. NCCR ilipokua na nguvu mliisingizia, CUF ilipojaribu kufurukuta mkachonga visu na mapanga mkapaka rangi ya cuf mkapeleka
    msikitini mkasema CUF magaidi na wanajificha
    msikitini. nani wa cuf alikamatwa kwa kuleta
    mapanga. CUF ni majuha wtengeneze mapanga
    wapake rangi yao. ndio vyombo vyetu hivyo
    Umeenda shule watambue wa TZ wa leo sio wale

    ReplyDelete
  9. wewe nape unauwezo gani wa kuwashughulikia watanzania wenzako? wewe ni nani? mmh! kumbe kuna magamba ya kiunoni ccm, sasa gaidi kati ya chadema na ccm ni nani?

    ReplyDelete
  10. nape tunaomba historia yako ulipo zaliwa, ulipokulia, na ulifikaje kwenye siasa? sisi tunakujua sana, kabla hujawashughulikia chadema tutakushughulikia wewe kwanza, na hao wanafamilia wenzako wa ccm,

    ReplyDelete
  11. Jamani Tumwache huyu Nape na siasa zake za maji machafu, mwenyewe anaogopa mahakama ila ni mchokozi, ngoja azid kuita wenzanke magaid uone. Gaid ni CCM na CCJ siyo CHADEMA, we sema unataka kujisafisha msaliti mkubwa

    ReplyDelete