15 November 2011

Lema akubali dhamana

Imeandaliwa na  Pamela Malel,Quine Lema na Richard Konga

Asema wataandamana bila kibali cha polisi

HATIMAYE Mbunge wa Arusha mjini Bw. Godbless Lema, (CHADEMA) ameaga mahabusu baada ya kukaa kwa takriban siku 14 baada ya kukubali kuwekewa dhanama katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa mkoani huo jana.


Awali Mbunge Lema alikataa dhamana kwa kile alichodai kuwa ni kwenda kutetea haki na kuchoshwa na kwa kile alichodai kuwa ni unyanyasaji na ukandamizaji wa haki za wananchi.

Mbunge huyo aliwekewa dhamana na wafanyabiashara wawili Bi. Sara Mohamed na Mwajuma Maamonge saa 3.14 asubuhi baada ya kukidhi matakwa ya dhamana iliyomtaka mweka dhamana kuwa na kitambulisho kibachotambulika kisheria na barua ya serikali ya Mtaa au Kijiji.

Awali akisomewa mashitaka mbHaruna Mataganeele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha Bi. Judith Kamala, mwendesha mashitaka wa serikali Bw. Haruna Matagane, huku Bw. Lema akitetewa na wakili wale Bw. Method Kimomogoro, alisema upande wa jamhuri hauna pingamizi la dhamana na kwamba mshitakiwa mwenyewe ndiye aliyekataa tangu awali.

Kwa upande wake wakili wa Lema alisema Novemva 7, mwaka huu alipokea barua ya mahamaka kumtaka awasilishe ombi la kuwa na wadhamini wawili kutoka kwa lema na kwamba alifanya hivyo jana hivyo kuomba mahakama iumpe dhamana mtekja wake jambo ambalo halikuwa na pingamizi lolote.

Muda mfupi baada ya mbunge huyo kutoka mahakani hapo alilakiwa na wafuasi wake na kubebwa juu juu huku yeye Bw. Lema akigeuza kibao toka kwa Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha na kumshutumu vikali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Magesa Mulongo.

Katika madai yake alisema mkuu huyo wa Mkoa ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, lakini yeye kama mbunge amechaguliwa na wananchi kwa kura 56,000 hivyo kujigamba kuwa na nafsi kubwa zaidi ya kiongozi huyo.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutoka gerezani Mbunge lema alisisitiza kuwa wataendelea kuandamana hata bila kuomba kibali polisi kwa madai kuwa ni kutetea haki za wananchi.

Mbunge huyo pia alidai kuwa alichoona mahabusu ni mambo ya kutisha ikiwemo watu bubambikiziwa kesi za ubakaji na kwamba baadhi ya watu wako humo kwa kukosa faini au dhamana ya sh. 20,000 au 35,000.

"Ngoja kama hawatakidhi vigezo sisi tutaandamana tena bila hata kibali kwa kuwa lengo letu si kuomba na kubembeleza amani bali lengo letu ni kutaka kila mwananchi aweze kupata haki kwa maana hiyo nasema kuwa maandamano lazima hapo yawepo,"alisisitiza Bw. Lema.

“Kama mkuu wa mkoa amekuja kwa mtazamo tofauti nawaambia hataweza, akithubutu kupambana kuzima haki na ukweli hataweza, yeye ameteuliwa na Rais sisi kama wabunge tumechaguliwa na watu,”aligamba mbunge Lema.

Alidai mkuu huyo wa mkoa kupelwaka Mkoa wa Arusha bila kuujua kwa undani mgogoro wa mji huo.

Alidai kuwa kiongozi huyo ni mgeni ambaye amewasili mkoani arusha bila kutambua matatizo ya msingi yaliyopo huku akifafanua kuwa mgogoro wa umeya arusha ndio uliopelekea waziri Mkuu Mizengo Pinda kusema uwongo bungeni.

“Huyu ni mgeni hapa Arusha hajui matatizo ya Arusha tatizo ni mgogoro wa umeya ambao ulimpelekea waziri mkuu kusema uwongo bungeni,”alidai.

Hatahivyo,alifafanua maisha yake wakati akiwa ndani ya gereza la Kisongo mkoani hapa kuwa alikutana na mambo ambayo mengine yanasikitisha kwa kuwa aliwakuta baadhi ya watu wakishikiliwa kwa kipindi kirefu kwa kukosa dhamana ya kiasi cha sh,20,000 kama faini.

Akisimulia kwa udnai alichodai kuona mahabusu alipokiwa gerezani alisema alikutana na kikongwe mwenye umri wa miaka 85 ambaye anatumikia jela kwa kukosa kulipa kiasi cha sh,35,000 kama faini huku akisisitiza kuwa asilimia kubwa ya watu waliopo jela wamesingiziwa kesi mbalimbali zikiwemo za ubakaji.

"Sasa kama imeshindikana na Rc (Mkuu wa mkoa) ndio huyo anaendelea kutukandamiza kwa kutoa matamko ambayo yanaonekana wazi kuwa anakipendelea zaidi chama tawala sasa ni bora wanawake kwa wanawake waende wakaongelee suala la mkoa wa arusha labda litaleta manufaa na kisha watuletee sisi kama wauem zao,"alisema Bw. lema.

Akiznguzmia kukaa kwake dhamana awali aliwataka wananchi kutambua kuwa yeye si mwehu kukataa dhamana na badala yake wanatakiwa kujua kuwa anatafuta haki ambayo inaondolewa na baadhi ya vyama vya siasa pamoja na Jeshi la polisi.

Alisema kuwepo kwake Gerezani ameweza kugundua na kujua kuwa ndani ya jeshi la polisi na kudai kuwa wapo baadhi ya askari ambao wanakiuka taratibu za jeshi hilo na kuwapa watu kesi ambazo si za kwao hali ambayo inasababisha madhara makubwa kwa wananchi hasa wale wenye kipato cha chini.

"Kwenda gerezani nimeweza kujua mambo mengi sana, kule kuna watu ambao wanasingiziwa kesi kwa kuwa baadhi ya watu wana ela sasa kama hali hii itaendelea kwa nchi hii haki itakuwa wapi kama sio wanyonge wote wataishia magereza na wale wenye hela wataachiwa huru jamani,"alidai.

3 comments:

  1. Ni kweli kabisa huyu Mkuu wa Mkoa Bw. Magesa Mulongo bado mgeni sana katika Jiji la Arusha. Ila ninasikitika kwani lengo lililomleta hapa la kuua CHADEMA kama alivyowaeleza viongozi wa CCM hapa Arusha alipopita kutambulishwa kwao halitatimia kwani ameshaonyesha udhaifu bado na mapema. Huwezi kuingia mji wa watu na ubabe kama alivyouonyesha ukafanikiwa. Kamwe hatafanikiwa kila mtu ameshamshtukia na kumdharau hata hao wana-CCM wenyewe wameshamshtukia kwa sababu wao wanasema anawagawa. Alitakiwa kwanza kufanya utafiti wa chanzo cha mgogoro ni nini? Badala yake ameingia kwa kutamba mno. Kwani yeye ndiye RC wa kwanza Arusha? Wamepita wengi na wataendelea kuletwa wengi anachotafuta ni presha tu na ataipata. Hii ni Arusha bwana uliza utaambiwa

    ReplyDelete
  2. lema ni kichaa,na sini shida yoyote kutoa pendekezo la kupimwa kicwa kama kiko sawa.

    ReplyDelete
  3. tunajua kuwa lema alishawahi kuwa jambazi sugu hivyo aligoma lkutoka gerezani ili kukutana na majamabazi wenziwe sugu ma kuwaweka sawa wasimtaje katika baadhi ya mambo makubwa aliyoyafanya lakini kikubwa KICHWA CHAKE NINA WASIWASI NACHO!!! KINA MATATIZO' mkyy wa mkoa chapa kazi usishindane na vichaaaaaaaaaa achana nae!!!!!! Asnat.

    ReplyDelete