15 November 2011

Bungeni kwachafuka

CHADEMA wasusia muswada, watoka nje, Mbowe kutangaza msimamo wao leo, Makinda awajibu wanaharakati.


Muswada wa Sheria ya kuundwa kwa Tume ya kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya umerudisha hali ya kutofahamu na utata katika Bunge la Tanzania kwa mara nyingine hali inayotafsiriwa kuwa ni kuzidi kuwachanganya watazania wa kawaida.

Hali ya kutofamu na utata uliibuka bungeni muda mfupi baada ya Waziri wa Sheria na Katiba Celina Kombani, kuwasilisha muswada huo kisha kuacha nafasi kwa hatua zinazofuata za Kamati na kambi ya upinzani kutoa maoni kabla ya kuanza kwa mjadala.

Baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani walitaka mwongozo wa Spika Anne Makinda, wakati Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Bi. Pindi Chana, alipokuwa akiwasilisha maoni ya kamati yake hali iliyomfanya Spika kukataa kupokea ombi hilo kwa muda huo.

Kutokana na hali hiyo mara baada ya juhudi hizo kugonga ukuta wabunge wa kambi ya upinzani wakionmgozwa na CHADEMA waliamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge na kueleza wazi kuwa hawatashiriki tena shughuli yoyote ya muswada huo kwa kuwa wamenyimwa nafasi ya kutoa maoni.

Hatua hiyo ya wabunge hao kutoka nje ya ukumbi wa bunge ilikuja muda mfupi baada ya Mbunge wa Singida Mashariki Bw. Tundu Lissu, (CHADEMA) kumaliza kuwasilisha maoni ya kambi hiyo na Spika Makinda kumwita mchangiaji wa kwanza Mbunge wa Wawi Bw. Hamad Rashid Mohamed ambaye hakuwepo.

Nafasi ya Bw. Mohamed ilichukuliwa na mchangiaji wa pili Mbunge wa Same Mashariki Bi. Anne Kilango Malecela, ambaye alipata wakati mgumu kuanza kuchangia kutokana na kutokea sauti za kuomba mwongozo mfulizo bila kufuata utaratibu.

Akizungumza nje ya ukumbi huo muda mfupi baada ya kuongoza wabunge wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi kutoka nje wa ukumbi wa Bunge Mkuu wa kambi hiyo Bw. Freeman Mbowe, alisema hawatashiriki tena muswada huo kwa kuwa hauna faida.

"Hatutashiriki tena katika suala zima la mchakato wa Katiba,"alisema Bw. Mbowe.

Alisema haiwezekani kuendelea kuvumilia kile alichokiita kuwa ni uonevu na badala yake kuahidi kutoa tangazo rasmi ambalo litakuwa linaonesha ratiba zao za kazi tofauti na mijadala ya katiba leo ili wananchi wajue kinachoendelea.

"Kesho (leo) tutatoa ratiba rasmi ya nini tutakuwa tunakifanya kwa umma,
kwa kuwa hatutashiriki katika hatua yoyote inayohusiana na mjadala huu wa
Muswada wa katiba, hakika tumechoshwa vya kutosha, sisi tutarudi kwa wananchi tuwaeleze tunataka kufanya nini,"alisema Bw. Mbowe bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Alisema walifikia uamuzi wa kutoka nje ya bunge baada ya kile alichokiita kuwa ni Spika Makinda kutowajali pindi wanapotaka kuomba muongozo.

Kwa upande wake Mbunge wa Kigoma Kusini Bw. David Kafulila, (NCCR-Mageuzi) alisema wameamua kuungana na CHADEMA kutoka nje kama hatua ya wazi kuonyesha kutokubali kitendo cha Spika kukataa kupokea kwanza mwongozo kabla ya kuruhusu hatu inayofuta.

"Tumeomba mwongozo wa spika mara nyingi amekataa kutusikiliza,"alisema Bw. Kafulila.

Naye Mbunge wa Muhambwe Bw. Felix Mkosamali, (NCCR Mageuzi ambaye pia alitoka nje ya ukumbi wa bunge alidai tangu awali Spika Makinda alikataa kuwapa nafasi ya kwenda kwa wananchi kukusanya maoni yeye akiwa kama mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo.

"Tatizo la Spika tangu awali alikataa kukubaliana na maoni ya wanakamati ya
Katiba Sheria Mbunge kwenda kukusanya maoni ya wananchi, kila wakati alidai yuko nje,"alisema Bw. Mkosamali.

Spika Makinda anena

Hata hivyo katika majumuisho yake Spika Makinda alikanusha lawama hizo na kueleza bunge kuwa hajakataza mbunge yeyote kwenda kwa wananchi kukusanya maoni na kwamba hatu hiyo bado haujafikiwa.

"Jamani waheshimiwa wabunge, bunge linaendeshwa kwa kanuni, huu ni mwaka sasa kutumia kanuni zetu hizi, kama mtu anataka kuleta hoja atumie kanuni zetu.

"Mimi sijakataa wabunge kukusanya maoni ya wananchi, lakini muda huo bado ndio tunataka tufike huko, kila mmoja atapata nafsi ya kusema kile anachotaka,"alisema.

Katika hali iliyoonesha dalili ya kutaka kuweka mambo sawa Spika Makinda alitoa maneno ya utangulizi kwa kujibu shutuma za wana haratati zilizotolewa Jijini Dar es juzi katika mdahalo uliandaliwa na Jukwaa la Katiba kuwa wananchi hawakushirikishwa na kwamba muswada huo ulitakiwa kuwasilishwa kwa mara ya kwanza na sio mara a pili.

Alisema awali kilichotakiwa ni kufanya marekebisho kwa kuongeza michango ya wabunge na wananchi na si kufuta muswada huo na kuanza hatua za mwanzo kwa kwamba kama wangefanya hivyo wangekwenda kinyume cha kanuni za bunge.

"Maoni ya wananchi yalikusanywa ikiwemo Dar es Salaam na Zanzibar, lakini pia kinachofanyika sasa ni kukusanya maoni kuwawezesha wananchi kutoa maoni yao, kila mtu atapata nafsi ya kutoa maoni yake, bila kupitishwa na bunge wananchi hawawezi kutoa maoni yao.

"Kwa mujibu wa kanuni ya 86 ya bunge inaruhusu muswada huu kusomwa kwa mara ya pili baada ya kupelekwa kwa tume ya Bunge,Sheria, Katiba na Utawala Bora,wadau walishirikishwa na kutoa maoni yao, hata hao waliozunguza walileta maoni yao,"alisema Spika Makinda na kuongeza.

"Kanuni ya 80,86 na 88 imekidhi matakwa yote. lazima uingie hatua ya pili kwa kuwa tayari lifafanyika, tusiwapotoshe wananchi, tuwe wakweli, na sasa nawaomba tuzingatie kanuni zetu,"alisema.

Anne Kilango aja juu

Katika mchango wake akiwa kama mchangiaji wa pili japo wa tatu kiratiba baada ya Bw. Mohamed kutokwepo Mbunge wa Gando Khalifa Suleman Khalifa (CUF), alishaa baadhi ya wabunge wenzake kutomheshimu Rais wa nchi kwa kutotambua nafasi yake katika kuteu wajumbe wa Tume hiyo kwa kushauriana na watu wake.

Alisema Rais wa nchi ni mkuu wa nchi, ni kiongozi mkuu, ni amiri jeshi mkuu hivyo ni lazima awe na nafasi yake na kuhoji uhalali wa nafasi hiyo ya rasi sasa kujadiliwa kwa undani zaidi.

"Si kwamba hata mtu akifanya jambo zuri lakini kwa kuwa amefanya fulani eti hilo halifai, hii si haki, kutokana na marekebisho yaliyofanyika nakubali kuwa kuna juhudi kubwa zimefanyika,"alisema Bw.Khalifa

Akizungumzia nafasi ya Tanzani visiwani mbunge huyo alionesha dalili ya kukasirishwa na CHADEMA kutoitambua eneo hilo la muungano katika mchakato huil na kudai kuwa chama hicho haina dhamira njema na muungano wa nchi.

Katika mdahalo wa juzi Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba,  alitoa msimamo wa kuitaka serikali kusoma muswada huo kwa mara ya kwanza na kudai kuwa wataandaa maandamano ya nchi znima yasiyokoma iwapo utawasilishwa kwa mara ya pili.

Hata hivyo baadhi ya watanzania wamekuwa wakipotosha ukweli kuhusu muswada huo huku wakiwachanganya wananchi kuwa huo ni sawa na uundwaji wa katiba yenyewe kutokana na michango yao na hoja wanazotoa mbele ya wananchi.

Tayari Rais Jakaya Kikwete, amewahakikishia Watanzania kuwa hatamaliza muda wake mwaka 2015 bila kuwaachia Katiba Mpya na kuweka wazi kuwa kazi hiyo itakamilika mwaka 2014.

3 comments:

  1. KIKWETE MWONGO
    ANAZUGA KUTAKA KATIBA MPTA HUKU PEMBENI AKIMTAKA SPIKA ANA MAKINDA AMINYE MAKALI YA WABUNGE KATIKA KUUJADILI MUSWAADA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA.
    UNAFIKI TUPU BUNGENI

    ReplyDelete
  2. Jamani mumesahau waliopanda ndege kurejesha fomu Dodoma mwaka uleee! Walikuwa ni Kikwete, Lowasa na Makinda! Hapo ndipo Mwalimu akaingilia kati kumwengua Kikwete na kumpa Mkapa. Mkapa kwa hasira akambwaga Makinda kusini kuwa Mkuu wa Mkoa akaachia Uwaziri! Sasa Boyz 2 Men wako Ikulu Makinda karudi kama moto wa nyika! Kila kitu choma bora Boyz 2 Men wapete! Kidudu mtu mmoja kanitonya 2015 Raisi Mwanamke! Kisia wee mwenyewe ni nani! Lowassa anazuga tu; wao wenyewe weshamchagua 'Sister'! Lowassa hauziki tena kwa hiyo bidhaa sasa ni 'sister' subirini mtaona mbele ya safari! Eti wanadhani wanawake woote watamkubali kwa kuwa tu kachanika katikati ya miguu! Huu si uspika, wote tutapiga kura kumchagua Raisi 2015 na hatutaangalia maumbile bali uadilifu, usafi wa matendo na kauli, umri, uzalendo, hekima, utiifu wa utawala wa sheria na busara. Kamwe hatutampigia kura mwenye sifa ya kubinya demokrasia, mwenye jeuri ya kufunga barabara, kapera, anayejiuza ili apate cheo, n.k.

    ReplyDelete
  3. tatizo wa-tz hamjazoea kuona mijadala moto ya mabunge mengine duniani, mfano mdogo tu tizameni bunge la india ndio mtajua nini nazungumzia hapa! dodoma cha mtoto tu! Zoeeni tu tena, mtaisoma namba

    ReplyDelete