16 November 2011

Wasamaria jitokezeni kumsaidia Abdallay

Na Anneth Kagenda

Bw. Shaban Abdallay

KIJANA Shabani Abdallay (26) Mkazi wa Gongo la Mboto Mzambalauni amewaomba wafadhiri na viongozi mbalimbali kujitokeza
kumsaidia kwa kumpatia mtaji wa kuuza vocha kutokana na ugonjwa wa tende la nguu alionao ambao hawezi kufanya kazi yoyote.

Akizungumza mara baada ya kufika kwenye Ofisi za majira zilizopo mtaa wa Lugoda Dar es Salaam jana, Abdallay alisema kuwa tatizo la mguu huo ni moja ya sababu kubwa ambayo imekuwa ikimsababisha kutofanya kazi yoyote hivyo kuwa tegemezi kwa ndugu na jamaa.

Alisema kuwa siyo ndugu wote wenye moyo wa huruma, hivyo kusababisha ndugu wengine kumuona ni kero na ndio maana aliamua kufika kwenye ofisi hizi kwa ajili ya kuomba msaada kwa mtu yeyote ili aweze kujishughulisha na badaye kupata kipato cha kuweza kujikimu kwenye maisha yake.

Alisema kuwa pamoja na msaada huo wa kuuza vocha vile vile anaomba ikiwa anaweza kujitokeza mfadhiri ambaye anaweza kumsaidia kupata matibabu ya kuwa akiudhuria kriniki ndani ya miaka mitatu ili mguu huo uweze kunywea.

"Mguu huu ulianza kuvimba taratibu tangu mwaka 2000, nimezunguka katika mahospitali mbalimbali ikiwamo, Ocean Road, Amana, Hospitali ya Tumbi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na nyingine nyingi lakini nilipoenda katika  Hospitali ya Macho ya CCBRT walinieleza kwamba Tende haiwezi kupona badala yake nitumie dawa kwa muda wa miaka mitatu ili kuweza kupunguza maumivu na homa kali ninayoipata lakini mguu hauwezi kunywea," na kuongeza

"Hivyo basi baada ya kupata majibu ya kukatisha tamaa nikaamua nikae nyumbani lakini naona ninavyozidi kukaa umri unaenda, hivyo inaweza kufikia mahari nikakosa kabisa mtu wa kunisaidia lakini nikipatiwa mtaji nitaweza kujikwamua na kuondokana na hali ya kuwa ombaomba," alisema Abdallay.

Aidha alisema kuwa pamoja na kuomba mtaji huo lakini kama kuna uwezekano wa matibabu anaomba mfadhiri yeyote kujitokeza kwani amekuwa akisumbuliwa na homa za mara kwa mara pamoja na maumivu makali kwenye mguu huo uliovimba.

Hata hivyo alisema kuwa hali ya maisha yake kuwa magumu pia imechangiwa zaidi na kufariki kwa wazazi wake na kusema kwamba marehemu mama yake ambaye alikuwa akimsaidia alifariki mwaka 2006 wakati baba yake alifariki mwaka 2009.

1 comment:

  1. Abdallah, huhitaji pesa ila uponyaji. Na ikiwa ni KWELI unahitaji msaada, msaada hautoki kwa watu wala wanadamu, ila kwa MUNGU pekee.
    Ikiwa KWELI unahitaji kusaidiwa na kupona, njoo KANISA LA SILOAMU, Mbezi Beach, shuka kituo cha Makonde, ulizia kanisa la SILOAMU, hapo ndipo MUNGU aliyekuumba wewe ukiwa mzima, atakurejeshea UZIMA wako, naye ni Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, ambaye HAKIKA kwa jina la YESU KRISTO yeye atakuweka HURU ( Matendo 10:38 ).

    Huo sio ugonjwa wala sio tende, hilo ni JOKA la MIZIMU limekutanda mguuni,na wala sio homa ila ni MAJINI tu, sasa hata uende India au Marekaji au CCBRT au Ocean Road, hata uende Ikulu au mganga awaye yote, hawatakusaidia lolote, ila ni YESU KRISTO pekee.

    Nenda, ukatubu na UOKOKE. Full Stop. Mwenye MASIKIO na ASIKIE. Yupo MUNGU wa ELIYAH (1 Falme 18:36-40), yeye hashindwi na jambo lolote, yeye ni MUNGU WA MAJESHI (anapigana vita hata kupitia ujumbe huu sasa)

    NARUDIA: ABDALLAH kama KWELI unataka kupona, nenda kanisani (sio dini) ila kanisani, nenda SILOAMU CHURCH...pasipo kufanya hilo, nasema POOOOOLE sana

    ReplyDelete