17 November 2011

Kaseja ampa tano nahodha Chad

Na Shufaa Lyimo

MLINDA mlango namba moja wa Simba na Taifa Stars, Juma Kaseja ameusifu uchezaji wa nahodha wa timu ya Chad, Mahamat Habib kutokana na jinsi anavyojua kupeleka mashambulizi langoni mwa wapinzani.
Kaseja aliyasema hayo jana kupitia kipindi cha michezo ya redio moja nchini, wakati alipokuwa anazungumzia mipango ya mechi zijazo.

Alisema mchezaji huyo anacheza mpira wa kulipwa nchini Tunisia, hivyo alitumia uzoefu wake kumsumbua walipocheza juzi jijini Dar es Salaam katika mechi ya kufuzu hatua ya makundi kuelekea fainali za Kombe la Dunia 2014, na Stars kufungwa bao 1-0.

"Nahodha wa Chad alinisumbua sana kwa sababu anajua kushambulia vizuri, amenipa changamoto ya kujipanga vyema katika kundi tutakalopangiwa," alisema Kaseja.

Licha ya Stars kufungwa bao hilo, timu hiyo imefanikia kuingia hatua ya makundi, kutokana na kuifunga Chad mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Jumamosi jijini N'djamena.

No comments:

Post a Comment