BRAZILIA, Brazil
MCHEZAJI wa kiungo wa Real Madrid, Ricardo Kaka atakosa mechi za kirafiki za Brazil dhidi ya Gabon na Misri, sambamba na Marcelo kutokana na kuwa majeruhi.
Shirikisho la Soka la Brazil (CBF), lilithibitisha juzi kuwa wawili hao wameondolewa katika mechi hizo zijazo.
Mchezaji wa zamani wa Milan, Kaka anaumwa kisigino wakati Marcelo ametolewa kwa kuwa na maumivu ya msuli.
Kaka hajaichezea timu ya taifa lake kuanzia Julai mwaka jana, wakati Selecao ilipoondolewa katika michuano ya Kombe la Dunia Afrika Kusini kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Uholanzi.
CBF pia imetangaza kwenye mtandao wao kwamba Luiz Gustavo, atacheza mechi dhidi ya Gabon.
Nyota huyo wa Bayern Munich, hana hati ya kumwezesha kwenda Gabon na atajiunga na timu wakati ikijiandaa kwa mechi nyingine.
Brazil itapambana na Gabon mjini Libreville kesho, wakati mechi dhidi ya Misri itachezwa Jumatatu ijayo nchini Qatari, katika mji mkuu wa Doha.
No comments:
Post a Comment