11 November 2011

Igeni mfano wa TCRA - Waziri

Na Neema Malley

WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, amezitaka taasisi mbalimbali nchini kuiga mfano wa Mamlaka ya Udhibiti  Mawasilino Tanzania (TCRA) kutoa ufadhili kuwasomesha wanafunzi watano kwenye ngazi tofauti ya elimu ya juu ili kuiezesha taifa kuwa na wataala wa kutosha wa sayansi.


Prof. Mbarawa alisema hayo jana kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya wizara yake katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam na kuziomba taasisi za serikali na binafsi kuchangia maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini kwa kutoa udhamini katika sekta hiyo.

Alitoa Tuzo ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu kwa wagunduzi na wabunifu mbalimbali waliofanya vizuri zaidi kama utambuzi rasmi wa serikali kwa wadau hao kuendeleza sayansi na teknolojia kwa njia ya ubunifu.

Waziri huyo pia alitoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa katika masomo ya sayansi kati ya mwaka 2010 na mwaka huu katika mitihani ya kidato cha nne.

Zawadi hizo ni cheti pamoja na fedha taslimu sh. 800,000 wakati wanafunzi waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita wakipewa kompyuta ya mkononi (Laptop) pamoja na cheti.

Waziri Mbarawa kwa kuthamini mchango wa walimu kuwawezesha wanafunzi hao kufanya vizuri katika masomo yao ya sayansi kitaifa aliwapa zawadi ya cheti ya fedha kiasi cha sh. 200,000. walimu hao walitoka katika Shule za Kifungiro, Babrojonsoni, Royola, Tabora na Ilboru.

No comments:

Post a Comment