Na Shufaa Lyimo
KUNDI la muziki wa taarabu la Five Stars, linatarajia kufanya ziara katika mikoa ya Kusini kuanzia Novemba 24 hadi 27, mwaka huu kwa lengo la kutoa burudani kwa mashabiki wao.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizo Dar es Salaam juzi, Ally Kijoti, alisema wameamua kufanya ziara hiyo baada ya kupata maombi mengi kutoka kwa mashabiki wao waliopo mikoani humo.
"Mashabiki wetu wa mikoa ya Kusini wakae sawa, ili kusubiri burudani za aina yake kutoka kwetu, licha ya kuwa wenzetu wametangulia mbele ya haki hakuna kilichoharibika bado tunakandamiza kama kawaida," alisema Kijoti.
Alisema sehemu watakazotoa burudau ni Masasi, Newala, Nachingwea, Mtwara pamoja na Lindi.
Kiongozi huyo alisema, anaendelea kuwashukuru wapenzi wa kundi lake kwa ushirikiano wanaowapa.
Kundi hilo liliondokewa na baadhi ya wasanii wake, baada ya kupata ajali ya gari wakati wakitokea Songea, ambako walikwenda kutumbuiza.
No comments:
Post a Comment