21 November 2011

Castle yatia mkono Ligi Kuu Uingereza

Na Victor Mkumbo

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Castle Lager, imedhamini kuonesha Ligi Kuu ya Uingereza (Barclays) kwenye vituo 48 vya televisheni barani Afrika.


Akizungumza na waandishi wa habari juzi Dar es Salaam, Meneja wa bia hiyo, Kabula Nshimo alisema wameamua kudhamini ligi hiyo ili kutoa fursa kwa mashabiki wa timu za Ulaya kushuhudia mechi mbalimbali na kushangilia timu wazipendazo.

Alisema hii ni mara ya pili mfululizo kwa bia hiyo kudhamini kuonesha mechi za Barclays kwa vituo mbalimbali vya televisheni Afrika.

Alisema hiyo ni moja ya sehemu ya kusaidia uendeshaji wa matukio ya michezo katika bara la Afrika kwa ajili ya kuwathamini washabiki wa mpira wa miguu.

Kabula alisema mashabiki soka watapata fursa ya kuangalia mechi mbalimbali kila siku ya  Jumamosi, ambazo zitahusisha ligi hiyo.

“Castle imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika soka kwa kipindi cha miaka 30 hadi sasa, ikiwa inadhamini michuano ya Kombe la Chalenji, Kombe la Kagame pamoja na Ligi Kuu ya Afrika Kusini,”  alisema.

No comments:

Post a Comment