21 November 2011

Wezi wa mifugo wadaiwa kuchoma nyumba ya Kamanda

Na Timothy Itembe Tarime Mara

MKAZI wa Kijiji cha Kwisarara wilayani Tarime, Mkoa wa Mara Bw. Machero Ghati, (33) amenusurika kufa baada ya mji wake kuteketezwa na mto na watu wanaoaminika kuwa ni wezi wa mifugo wanaokasirishwa na msimamo wake wa kupinga wizi huo.


Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa 8 usiku wa kumakia jumamosi.

Bw. Ghati ambaye pia ni Kamanda wa sungusungu Tarime na Rorya anayetakiwa kusimamaia kumalizika kwa wizi wa mifugo uliokithiri na kudaiwa kufanywa na jamii ya kikurwa dhidi ya wajaluo wa Rorya anaelezwa kuwakera wezi wanaoaminika kupita katika kata hiyo baada ya kuiba katika Wilaya ya Rorya.

Akisimulia tukio hilo kwa njia ya simu, kamanda huyo wa sungusungu alisema siku ya ijumaa saa 8 usiku alishitukia watu takriban wanne wakiingia nyumbani kwake huku wakimtaka kujitokeza ili wamuue.

Alisema baada ya kusikia sauti hiyo ghafla aliamka na kujimbaza ili wasimwone na muda mfupi alishitukia nyumba zake zikianza kuwaka moto.

Kamanda Polisi wa Mkoa maalum ya kipolisi Tarime Rorya bw. Justus Kamugisha, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea Novemba 19 saa 8.5 usiku na kwamba nyumba zilizochomwa ni mbili za na kusababisha hasara ya sh. 693.000

Kamanda Kamugisha alitaja mali zilizoharibiwa na kusababisha hasara kuwa televishen moja aina ya panasoniki yenye thamani ya sh. 184,000 na kuongeza kuwa tivu vingine ambavyo kwa ujumla vina thamani ya sh. 693, 000 ni meza, viti na mali zingine.

Alisema mmoja ya watuhumiwa hao aliyetambuliwa kwa jina la Bw. Wankyo Marigo, wa kijiji hicho anasakwa na jeshi la polisi baada ya kutoroka.

Bw. Ghati alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kukomesha vitendo vya kutishia maisha ya wapambanaji wa wizi wa mifugo uliokithiri kwa kuwa vinaweza kuwavunja moyo wahusika kama yeye na wenzake.

Katika hatua nyingine Bw. Ghati amechangiwa fedha taslimu sh. 230,000 kama hatua ya wazi ya kutambua na kuthamini mchango wake ili aweze kupata mahala pa kujihifadhi pamoja na familia yake wakati huu mgumu.
           
Mpango wa kumchangia kamanda huyo uliibuniwa na Diwani wa Kata ya Kitembe Thomas Patrick, huku Mbunge wa Jimbo la Rorya Bw. Lameck Airo akichangia sh. 150,000, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Panya'koo Bw. Protest Matola,  akichangia sh. 50,000, Diwani wa Kata ya Goribe Bw. Lukasi Ongeto, akichangia sh.30,000.

Harambee hiyo iliyobuniwa ghafla muda mfupi baada ya taarifa hizo kuenea na voingozi hao kufika kujionea jinsi Kamanda huyo wa sungusungu alivyonusurika huku akifanyiwa unyama uliendana na wito kwa serikali kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kama kweli kuna nia ya kumaliza wizi wa mifugo.

No comments:

Post a Comment