24 October 2011

Yanga yaiua Oljoro Chamazi

*Yashika nafasi ya pili

Na Specirose Joseph

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, jana walishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, baada ya kuifunga JKT Oljoro bao 1-0 katika
mechi iliyochewa katika Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.

Yanga inashika nafasi pili kwa kuwa na pointi 21, sawa n*Yashika nafasi ya pili

Na Specirose Joseph

MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, jana walishika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, baada ya kuifunga JKT Oljoro bao 1-0 katika mechi iliyochewa katika Uwanja wa Azam Chamazi, Dar es Salaam.

Yanga inashika nafasi pili kwa kuwa na pointi 21, sawa na Azam FC isipokuwa zinatofautina kwa idadi ya mabao kufunga na kufungwa, huku JKT Oljoro ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 19. Simba inaongoza kwa kuwa na pointi 27.

Mabingwa hao walianza kwa kuliandama lango la JKT Oljoro, kwa dakika kumi za kwanza na kuwafanya mabeki wa wapinzani wao kufanya kazi ya ziada.

Dakika za saba na kumi Jerry Tegete, alifanya kazi ziada baada ya kupiga mashuti ya nguvu langoni mwa Oljoro, lakini mabeki wa maafande hao walikaa imara kuondoa hatari hizo.

Baada ya kushambuliwa mfululizo, JKT Oljoro ilizinduka dakika ya 18 na kufanya shambulizi la nguvu, kupitia kwa Ally Mkanga kupiga shuti lililopaa nje ya lango.

Yanga ilijibu shambulizi hilo dakika ya 19, Keneth Asamoah baada ya kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa wa JKT, Said Lubawa.

Dakika ya 30 Ally Shamte wa Yanga, alikosa bao baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya goli la JKT.

Katika kipindi hicho JKT Oljoro ilimtoa, Meck Chundi kutokana na kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Karage Mgunda.

Kipa wa Oljoro, Lubawa alifanya kazi ya ziada dakika ya 37, baada ya kupangua shuti kali la Haruna Niyonzima, ambaye alikuwa katika nafasi nzuri ya kufunga.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga, kufanya mashambulizi mengi lakini washambuliaji wake walioongozwa na Asamoah, hawakuwa makini katika kufunga.

Baada ya JKT oljoro kuona hali tete, ilifanya mabadiliko katika kipindi hicho cha pili ambapo alitoka, Mkanga na nafasi yake kuchukuliwa na Frank George.

Mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Mkuu wa Yang, Sam Timbe yalizaa matunda dakika ya 86 baada ya Hamis Kiiza, aliyeingia kuchukua nafasi ya Tegete kuipatia timu yake bao la ushindi.

Mara baada ya mechi kumalizika kocha Timbe, alisema amefurahi kupata matokeo hayo kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwani kila timu ilikuwa inatafuta ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri.
Mara baada ya mechi kumalizika kocha Timbe, alisema amefurahi kupata matokeo hayo kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwani kila timu ilikuwa inatafuta ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri.a Azam FC isipokuwa zinatofautina kwa idadi ya mabao kufunga na kufungwa, huku JKT Oljoro ikishika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 19. Simba inaongoza kwa kuwa na pointi 27.

Mabingwa hao walianza kwa kuliandama lango la JKT Oljoro, kwa dakika kumi za kwanza na kuwafanya mabeki wa wapinzani wao kufanya kazi ya ziada.

Dakika za saba na kumi Jerry Tegete, alifanya kazi ziada baada ya kupiga mashuti ya nguvu langoni mwa Oljoro, lakini mabeki wa maafande hao walikaa imara kuondoa hatari hizo.

Baada ya kushambuliwa mfululizo, JKT Oljoro ilizinduka dakika ya 18 na kufanya shambulizi la nguvu, kupitia kwa Ally Mkanga kupiga shuti lililopaa nje ya lango.

Yanga ilijibu shambulizi hilo dakika ya 19, Keneth Asamoah baada ya kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa wa JKT, Said Lubawa.

Dakika ya 30 Ally Shamte wa Yanga, alikosa bao baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya goli la JKT.

Katika kipindi hicho JKT Oljoro ilimtoa, Meck Chundi kutokana na kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Karage Mgunda.

Kipa wa Oljoro, Lubawa alifanya kazi ya ziada dakika ya 37, baada ya kupangua shuti kali la Haruna Niyonzima, ambaye alikuwa katika nafasi nzuri ya kufunga.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga, kufanya mashambulizi mengi lakini washambuliaji wake walioongozwa na Asamoah, hawakuwa makini katika kufunga.

Baada ya JKT oljoro kuona hali tete, ilifanya mabadiliko katika kipindi hicho cha pili ambapo alitoka, Mkanga na nafasi yake kuchukuliwa na Frank George.

Mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Mkuu wa Yang, Sam Timbe yalizaa matunda dakika ya 86 baada ya Hamis Kiiza, aliyeingia kuchukua nafasi ya Tegete kuipatia timu yake bao la ushindi.

Mara baada ya mechi kumalizika kocha Timbe, alisema amefurahi kupata matokeo hayo kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu kwani kila timu ilikuwa inatafuta ushindi ili kujitengenezea mazingira mazuri.

1 comment:

  1. Waandishi wa habari si muache kuandika. Jamani mbona mnasikitisha. Mmesoma vyuo gani nyie?

    ReplyDelete