24 October 2011

Man City yaikomoa Man United

*Yaichapa mabao 6-1

LONDON, Uingereza

MANCHESTER City, jana ilivunja mwiko wa mahasimu wao United wa kutofungwa katika Ligi Kuu England
msimu huu na kuipa kipigo kikubwa zaidi ya kile cha Februari 1955 kwa kuichapa mabao mabao 6-1 katika mechi iliyochezwa Katika Uwanja wao wa Old Trafford.

City katika miaka 56, iliyopita iliwahi kuichapa United mabao 5-0, lakini ushindi wa jana ulionesha kupiga kwao hatua dhidi ya United, ambao ni mabingwa wa Ligi England mara 19.

Kwa ushindi huo City imezidi kujichimbia kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu England kwa kufikisha pointi 25, huku United ikibakiwa na pointi 20 katika nafasi ya pili, kabla ya mechi kati ya Chelsea dhidi ya Queens Park jana.

Mshambuliaji wa Kitaliano mwenye asili ya Afrika, Mario Balotelli ndiye alianza kuifungia City katika dakika ya 22, baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa  James Milner.

Mchezaji huyo baada ya kufunga kama kawaida yake hakushangilia, alivua jezi yake kwa mbele na kuonesha maandishi yaliyosomeka WHY ALWAYS ME? (Kwanini kila wakati mimi?.

Bao hilo lilidumu kipindi chote cha kwanza, kipindi cha pili Balotelli aliongeza bao jingine dakika ya 60 kwa kupasiwa tena na Milner.

Manchester United ilijikuta katika wakati mgumu kwa kulazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya Jonny Evans, kutolewa kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu kwa kumwangusha Balotelli, aliyekuwa akielekea kufunga nje ya eneo la hatari.

Kutolewa kwa mchezaji huyo kulimfanya kocha wa United, Sir Alex Ferguson kufanya mabadiliko kwa kumwingiza, Javier Hernandez 'Chicharito' na Jones badala ya Luis Nani na Anderson.

Hata hivyo madadiliko hayo hayakuwa dawa kwa United, ambayo ilijikuta ikipachikwa bao la tatu na City dakika ya 69 kupitia kwa Sergio Aguero, aliyesiwa na Micah Richards baada ya kuanza kushambulia ikisaka mabao ya kusawazisha.

United ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa Darren Fletcher, aliyepiga shuti umbali wa yadi 20 baada ya kupata pasi ya Chicharito.

Mchezaji wa City aliyetokea benchi, aliyechukua nafasi ya Balotelli Edin Dzeko, alifunga bao la nne dakika ya 90 huku David Silva, akifunga la tano  dakika ya 91 na Dzeko kuongeza la sita dakika 93.

Katika mechi nyingine, Arsenal ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Stoke na kufikisha pointi 13 hivyo, kupanda hadi nafasi ya saba kutoka ya 10.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Gervinho (dk.27) na Van Persie (dk.73 na dk. 82 huku bao la Stoke liliwekwa kimiani na Peter Crouch dakika 34.

Everton ikiwa ugenini iliichapa Fulham mabao 3-1, mabao yake yalifungwa na Drenthe (dk.3),*Yaichapa mabao 6-1

LONDON, Uingereza

MANCHESTER City, jana ilivunja mwiko wa mahasimu wao United wa kutofungwa katika Ligi Kuu England msimu huu na kuipa kipigo kikubwa zaidi ya kile cha Februari 1955 kwa kuichapa mabao mabao 6-1 katika mechi iliyochezwa Katika Uwanja wao wa Old Trafford.

City katika miaka 56, iliyopita iliwahi kuichapa United mabao 5-0, lakini ushindi wa jana ulionesha kupiga kwao hatua dhidi ya United, ambao ni mabingwa wa Ligi England mara 19.

Kwa ushindi huo City imezidi kujichimbia kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu England kwa kufikisha pointi 25, huku United ikibakiwa na pointi 20 katika nafasi ya pili, kabla ya mechi kati ya Chelsea dhidi ya Queens Park jana.

Mshambuliaji wa Kitaliano mwenye asili ya Afrika, Mario Balotelli ndiye alianza kuifungia City katika dakika ya 22, baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa  James Milner.

Mchezaji huyo baada ya kufunga kama kawaida yake hakushangilia, alivua jezi yake kwa mbele na kuonesha maandishi yaliyosomeka WHY ALWAYS ME? (Kwanini kila wakati mimi?.

Bao hilo lilidumu kipindi chote cha kwanza, kipindi cha pili Balotelli aliongeza bao jingine dakika ya 60 kwa kupasiwa tena na Milner.

Manchester United ilijikuta katika wakati mgumu kwa kulazimika kucheza wakiwa pungufu baada ya Jonny Evans, kutolewa kwa kadi nyekundu kutokana na kumchezea rafu kwa kumwangusha Balotelli, aliyekuwa akielekea kufunga nje ya eneo la hatari.

Kutolewa kwa mchezaji huyo kulimfanya kocha wa United, Sir Alex Ferguson kufanya mabadiliko kwa kumwingiza, Javier Hernandez 'Chicharito' na Jones badala ya Luis Nani na Anderson.

Hata hivyo madadiliko hayo hayakuwa dawa kwa United, ambayo ilijikuta ikipachikwa bao la tatu na City dakika ya 69 kupitia kwa Sergio Aguero, aliyesiwa na Micah Richards baada ya kuanza kushambulia ikisaka mabao ya kusawazisha.

United ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa Darren Fletcher, aliyepiga shuti umbali wa yadi 20 baada ya kupata pasi ya Chicharito.

Mchezaji wa City aliyetokea benchi, aliyechukua nafasi ya Balotelli Edin Dzeko, alifunga bao la nne dakika ya 90 huku David Silva, akifunga la tano  dakika ya 91 na Dzeko kuongeza la sita dakika 93.

Katika mechi nyingine, Arsenal ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Stoke na kufikisha pointi 13 hivyo, kupanda hadi nafasi ya saba kutoka ya 10.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Gervinho (dk.27) na Van Persie (dk.73 na dk. 82 huku bao la Stoke liliwekwa kimiani na Peter Crouch dakika 34.

Everton ikiwa ugenini iliichapa Fulham mabao 3-1, mabao yake yalifungwa na Drenthe (dk.3),
Saha (dk.90), Rodwell (dk.90+3),
Fulham ilipata bao lake kupitia kwa Ruiz (dk.67).

No comments:

Post a Comment