Na Damiano Mkumbo, Singida
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal, amesema serikali itashirikiana na chama cha
Wasioona Tanzania na wadau wengine kutatua changamoto zinazoikabili.
Dtk. Bilal alisema hayo katika hotuba yake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya fimbo nyeupe yaliyofanyika kitaifa mjini Singida
mwishoni mwa wiki.
Kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Bi. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Bilal alisema serikali itaweka mazingira mazuri ili walemavu wasioona waweze kutumia vipaji vyao kikamilifu kwa
manufaa ya taifa kwa ujumla.
Kiongozi huyo wa kundi hilo katika jamii limebainisha kuwa lina uwezo mkubwa wa
kufanya kazi kutokana na maonesho ya shughuli mbali mbali kwenye maadhimisho hayo kama matumizi ya kompyuta, ushonaji wa nguo kwa kutumia cherehani, ufundi wa simu, ushonaji viatu, na ufumaji.
“Hii ni changamoto kwa serikali katika kuhakikisha kuwa inakidhi mahitaji ya wasioona yakiwemo ya Teknologia ya Mawasiliano (JTC),” alisema.
Kuhusu ajira aliwashauri waajiri wote nchini kuona umuhimu wa kuwaajiri vijana wasioona katika nafasi mbalimbali zinazowafaa, hiyo itawasaidia kujiajiri na kutoa mchango wao katika taifa lao.
Alikiri na kupokea kilio chao kuhusu kiwango kidogo cha ruzuku kinachotolewa
na serikali.
Akizungumzia upatikanaji wa fimbo nyeupe ambayo ni msaada mkubwa kwa wasioona, alisema mahitaji ni makubwa kulingana na ongezeko la idadi yao na kushauri mamlaka husika nchini kuhakikisha fimbo hizo zinapatikana kwa bei nafu.
No comments:
Post a Comment